Kamba Ya Kukaanga Wa Chembechembe Za Mkate (bread crumbs)

Kamba Ya Kukaanga Wa Chembechembe Za Mkate (bread crumbs)

   

Vipimo

Kamba wakubwa waliochambuliwa maganda - kiasi 25-30

Pilipili manga - 1 kijko cha supu

Chumvi - kiasi

Chembechembe za mkate (bread crumbs) - 1 gilasi

Mayai - 3

Mafuta ya kukaangia - Kisia

Namna Ya Kupika:     

  1. Baada ya kusafisha kamba na kuosha, weka katika chujio watoke maji. 
  2. Katika sahani ya shimo, au bakuli, piga mayai, tia chumvi na pilipili manga.. 
  3. Katika chombo kingine weka chembechembe za mkate (breadcrumbs) 
  4. Weka mafuta katika karai yashike moto.  
  5. Chovya kamba katika mayai kisha katika chembechembe za mkate, kisha kaanga katika karai hadi wageuke rangi. 
  6. Epua chuja mafuta wakiwa tayari.
Share