Akiwa Amemdanganya Mumewe Atakuwa Ametalikika (Talaka)?

 

SWALI

Assalam aleikum,
Nina watoto watatu nimezaa kila mwaka na watoto wangu wa wili wa mwisho nimezaa kwa operation.niko kwenye nchi ambayo sina msaada wowote kwa yeyote hata mume wangu hanisaidii sina nguvu za kuzaa kwa sasa watoto wangu bado wadogo. Mume wangu alinipa ruhusa kutumia family planning kwa miezi sita sasa amenilazimisha niwache kutumia. Nimemdanganya kumwambia kuwa nishawacha asema
kama sio ukweli ameniacha jee talaka imepita

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwish

Mas-ala ya family planning kwa dharura inaruhusiwa katika sheria ya Kiislamu lakini hapa si mahali pake kwani katika suala hili limejibiwa kwa kina katika viungo vifuatavyo:

Kupanga Uzazi Na Sio Kuzuia Uzazi

Njia Gani Inayopasa Katika Sheria; Kuzuia Au Kupanga Uzazi?

Kuzuia Mimba Na Madhara Yake

Inafaa Kufunga Uzazi Kwa Sababu Ya Umri Mkubwa?

20 Kuhalalishwa ‘Azl (Kuchopoa Kabla Ya Kushusha)

21 Kutofanya ‘Azl Ni Bora Zaidi

 Kuhusu mas-ala ya talaqa kwa hakika huwa mara nyingi wanaume wanachukulia ni kama mchezo lakini talaqa si jambo la mchezo hata ukisema kwa dhihaka huwa talaqa imepita. Ama wewe ukiwa umemdanganya na hiyo talaqa yake imeegemea kwenye sharti, hivyo sharti hiyo ikipatikana inakuwa talaqa imepita kama katika mfano uliotoa.

Kwa hivyo, nyinyi wawili si mume na mke tena lakini bado mnaweza kurudiana.

Hakika ni kuwa mume na mke wanatakiwa wawe makini na wawe wakweli baina yao la si hivyo ndoa itavurugika. Nasaha kwa dada yetu ni kuwa akae na mume wake amueleze ukweli na kuwa hatarudia kosa hilo ili waweze kurudiana kama mume na mke kama awali. Ikiwa miezi mitatu haijamaliza mume anaweza kumrudia bila mahari mapya wakawa wanaishi kama mume na mke. Lakini ikiwa miezi mitatu imepita itabidi mfunge nikaha upya na mahari mapya na kwa kuwa wewe ndio umefanya makosa na unataka kuishi na mumeo unaweza kumsamehe mahari hayo.

 

Baada ya hapo sasa kwa sababu za kiafya ambazo huenda zikakuletea shida unaposhika mimba itakuwa ni bora uweze kuzungumza na mumeo na umueleze shida unayopata. Ikiwa mumeo ni Muislamu mzuri na barabara itakuwa ni rahisi sana kuelewana na kukubalia kutumia njia ya kuzuia kizazi. Ikiwa pia mumeo ni binadamu basi atakufikiria na hatataka uingie katika shida.

 

Na nasaha nyingine ambayo inaweza kukusaidia katika kupanga uzazi ni kunyonyesha kwa muda wa miaka miwili ambapo itakufanya usiingie damuni kwa muda wa kunyonyesha hivyo kutoshika mimba. Japokuwa ufanisi wa kufanya hivi unapatikana kwa 50% peke ya wanawake. Wapo wanawake wanaonyoyesha na bado wanaingia ada yao ya mwezi kama kawaida.

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share