078-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Viumbe Vyote Vinawaombea Wanaofunza Watu Kheri

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 78

 

Viumbe Vyote Vinawaombea Wanaofunza Watu Mambo Ya Kheri

 

 

 

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ (رضي الله عنه) أنَّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((فضْلُ الْعَالِمِ عَلَى الْعَابِدِ كَفَضْلِي عَلَى أَدْنَاكُم))  ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ اللَّهَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَأَهْلَ السَّمَوَاتِ وَالأَرَض حَتَّى النَّمْلَةَ فِي جُحْرِهَا وَحَتَّى الْحُوتَ لَيُصَلُّونَ عَلَى مُعَلِّمِي النَّاسِ الْخَيْرَ)) رواه الترمذي  وقَالَ حَدِيثٌ حَسَنٌ.

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Umaamah(رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Ubora wa Mwanachuoni juu ya mfanya ‘Ibaadah, ni kama ubora wangu juu ya mwenye daraja ya chini miongoni mwenu)). Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema:((Hakika Allaah na Malaika Wake, na walio mbinguni, hata wadudu chungu waliomo katika mashimo yao, na hata samaki, wanawaombea maghfirah wanaowafundisha watu kheri)). [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Fadhila adhimu za mwenye elimu ya Dini kwamba viumbe vyote vinamuombea maghfirah.

 

 

2. Ukumbusho wa fadhila za mwenye elimu, mojawapo ya fadhila ni kwamba wamesifiwa ni waje wenye kumkhofu Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ  

Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa. [Faatwir (35: 28)]

     

 

Na kwamba wao pamoja na Allaah (سبحانه وتعالى) na Malaika Wake wanashuhudia Tawhiyd ya Allaah (عزّ وجلّ) kama Anavyosema Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى):

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

 

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan (3: 18)]

 

Na pia wenye elimu ya Dini wanapandishwa daraja za juu na Allaah (سبحانه وتعالى):

   

 يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ

Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu.  [Al-Mujaadalah (58: 11)]

 

Rejea pia: An-Nisaa (4: 83), Al-‘Ankabuwt (29: 49), Az-Zumar (39: 9).

 

 

3. Himizo la kutenda linalomfaa mtu nafsi yake na wenginewe, jambo ambalo litamnufaisha hata baada ya kufariki kwake.

 

Rejea Hadiyth namba (77).

 

 

4. Kutafuta elimu ya kufikia cheo cha mwalimu au Mwanachuoni ni bora zaidi kuliko ‘Ibaadah za naafilah (Sunnah), kwani ‘Ibaadah inamnufaisha mtu pekee, lakini elimu haimnufaishi pekee, bali hata wengineo.

 

 

5. Dhihirisho la kuwapa heshima ‘Ulamaa wa Dini yetu na wanafunzi na kuwaombea maghfirah na du’aa nzuri.

 

 

6. Hadiyth hii inahimiza na kutilia nguvu mno suala la kutafuta elimu na kufunza watu hadi kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema katika Hadiyth ifuatayo kwamba dunia imelaaniwa isipokuwa kumdhukuru Allaah na Mwalimu na mwanafunzi anayejifunza Dini:

 

 

عن أبي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( أَلاَ إِنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ مَلْعُونٌ مَا فِيهَا إِلاَّ ذِكْرُ اللَّهِ ، وَمَا وَالاَهُ ، وَعَالِمٌ أَوْ مُتَعَلِّمٌ)) الترمذي وقال: حَدِيثٌ حَسَنٌ 

Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: ((Zindukeni! Dunia imelaaniwa, kimelaaniwa kilichomo humo isipokuwa dhikru-Allaah (kumtaja Allaah) na jambo linalokaribiana na hilo (la kumtii Allaah), Mwanachuoni na anayejifunza [Dini])) [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan]

 

 

 

7. Fadhila tele za kutafuta elimu na kufundisha zimetajwa pia katika Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), miongoni mwazo ni zifuatazo:

 

 

عن أَبِي الدَّرْدَاءِ (رضي الله عنه) قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((مَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَبْتَغِي فِيهِ عِلْمًا، سَلَكَ اللَّهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ)) مسلم 

Imepokelewa toka kwa Abuu Ad-Dardaa (رضي الله عنه) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Anayetafuta njia ya kutaka elimu humo, Allaah Humpatia njia ya Jannah [Peponi])) [Muslim]

 

Pia:

 

عن سَهْل بنِ سَعد رَضيَ اللهُ عنهُ أنَّ النَّبيَّ صَلى اللهُ عليْه وسلم قال لعليٍ رضي اللهُ عنهُ: ((فواللهِ لأَنْ يَهْدِيَ اللهُ بِكَ رَجُلاً وَاحِداً خَيْرٌ لَكَ مِن حُمْرِ النَّعَم)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Sahal bin Sa'ad (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema kumwambia ‘Aliy (رضي الله عنه): ((Wa-Allaahi, Allaah Akimhidi mtu mmoja kupitia kwako, ni kheri kwako kuliko ngamia mwekundu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ لاَ يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا))  مسلم

 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Yeyote anayelingania katika uongofu, atakuwa na ujira mfano ujira wa anayemfuata, hatapunguziwa kutokana ujira huo chochote)) [Muslim]

 

Pia:

 

 عن إبْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا شَيْئًا فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَ فَرُبَّ مُبَلَّغٍ أَوْعَى مِنْ سَامِعٍ ‏)) الترمذي وصححه الألباني

 

Imepokelewa kutoka kwa bin Mas’uwd (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah Amnawirishe mtu aliyesikia kitu kutoka Kwetu naye akakibalighisha kama alivyosikia. Huenda anayefikishiwa akawa ana fahamu zaidi kuliko aliyesikia)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katka Swahiyh At-Tirmidhiy (2657), Swahiyh At-Targhiyb (89)]

 

 

Pia:

 

عن مُعَاوِيَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ)) البخاري ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Mu'aawiyah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Akimtakia khayr (mja Wake) Humpa ufahamu (elimu) katika Dini)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Rejea pia Hadiyth namba (16), (80).

 

 

 

Share