Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Kuuza Kitu Cha Wizi Au Kununua

Hukmu Ya Kuuza Kitu Cha Wizi Au Kununua

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

Wakati mtu anapoiba kitu chochote na akamuuzia mtu mwengine na hali ya kuwa mtu huyo anafahamu kuwa kitu hicho kimeibiwa, je, kuna dhambi juu ya hilo?

 

JIBU: 

 

Mwenye kujua kuwa kinachouzwa ni cha wizi, basi ni haramu kwa mtu huyo kukinunua. Na ni wajibu juu yake kumkemea mwenye kufanya hivyo.  Na amnasihi kukirejesha kwa mwenyewe. Na atake msaada kwa viongozi juu ya jambo hilo, ikiwa nasaha hazitonufaisha.
 

[Majmuw' Al-Fataawa Ibn Baaz, juz.19, uk. 91]

 

Share