011 - Huwd

 

 

   هُود

 

011-Huwd

 

 

011-Huwd: Utangulizi Wa Suwrah

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ﴿١﴾

1. Alif Laam Raa.[1] Kitabu ambacho Aayaat Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa waziwazi kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ﴿٢﴾

2.  Kwamba: Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.

 

 

 

وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ﴿٣﴾

3. Na kwamba: Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake, Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliokadiriwa, na Atampa kila mwenye fadhila (amali njema), Fadhila Zake (malipo yake).[2] Na mkikengeuka, basi hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.

 

 

 

إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٤﴾

4. Kwa Allaah ni marejeo yenu. Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٥﴾

5. Tanabahi! Hakika wao wanainamisha vifua[3] vyao ili wamfiche (Allaah). Tanabahi! Wanapojigubika nguo zao, Anajua wanayoyafanya siri na wanayoyatangaza. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.[4]

 

 

 

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦﴾

6. Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah, na (Allaah) Anajua mahali pake pa kustakiri na pa kuhifadhiwa kwake. Yote yamo katika Kitabu kinachobainisha.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ وَلَئِن قُلْتَ إِنَّكُم مَّبْعُوثُونَ مِن بَعْدِ الْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧﴾

7. Na Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, na ‘Arshi Yake ilikuwa juu ya maji[5], (kakuumbeni) ili Akujaribuni nani kati yenu mwenye amali nzuri zaidi. Na kama ukisema: Nyinyi mtafufuliwa baada ya mauti, wale waliokufuru bila shaka watasema: Hakika haya si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.

 

 

 

وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَىٰ أُمَّةٍ مَّعْدُودَةٍ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُ ۗ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٨﴾

8. Na kama Tukiwaakhirishia adhabu mpaka muda[6] uliokwishahesabiwa, bila shaka watasema: Ni nini kinachoizuia? Tanabahi! Siku itakayowafikia haitaondoshwa kwao, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ لَيَئُوسٌ كَفُورٌ﴿٩﴾

9. Na Tunapomuonjesha binaadam Rehma kutoka Kwetu, kisha Tukamuondolea, hakika yeye huwa ni mwenye kukata tamaa sana asiye na shukurani.[7]

 

 

 

وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ السَّيِّئَاتُ عَنِّي ۚ إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ﴿١٠﴾

10. Na Tunapomuonjesha neema baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: Maovu yemeniondokea. Hakika yeye ni mwenye kufurahi sana kwa kujigamba na kujifaharisha.[8]

 

 

 

إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١١﴾

11. Isipokuwa wale waliosubiri na wakatenda mema hao watapata maghfirah na ujira mkubwa.

 

 

 

فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَا أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿١٢﴾

12. Basi labda wewe utaacha baadhi ya yale uliyofunuliwa Wahy na kifua chako kitaona dhiki kwa hayo kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa hazina au hakuja pamoja naye Malaika? Hakika wewe ni mwonyaji tu, na Allaah Ni Mtegemewa wa kila kitu.

 

 

 

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾

13. Je, wanasema ameitunga (hii Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli.[9]

 

 

 

فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنزِلَ بِعِلْمِ اللَّـهِ وَأَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ﴿١٤﴾

14. Wasipokujibuni, basi jueni kwamba hakika (hii Qur-aan) imeteremshwa kwa Ujuzi wa Allaah, na kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Basi je, nyinyi mtakubali kuwa Waislamu?

 

 

 

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ﴿١٥﴾

15. Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu amali zao humo, nao hawatopunjwa humo.[10]

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٦﴾

16. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa moto. Na yataporomoka yale waliyoyafanya humo (duniani), na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴿١٧﴾

17. Je, basi yule aliye na hoja bayana kutoka kwa Rabb wake, na akafuatiwa na Shahidi[11] kutoka Kwake, na kabla yake (kilikuwa) Kitabu cha Muwsaa kilichokuwa kiongozi na rehma (je, huyo ni sawa na aliye kwenye giza la ukafiri?). Hao ndio wanaoiamini (Qur-aan). Na atakayeikanusha kati ya makundi, basi moto ndio mahali pa miadi yake. Basi usiwe katika shaka nacho. Hakika hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako, lakini watu wengi hawaamini.

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۚ أُولَـٰئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾

18. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia uongo Allaah? Hao watahudhurishwa mbele ya Rabb wao, na mashahidi watasema: Hawa ndio wale waliomzulia uongo Rabb wao! Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu.

 

 

 

الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿١٩﴾

19. Wale wanaozuia Njia ya Allaah na wanaitafutia upogo na wao ni wenye kuikanusha Aakhirah.

 

 

 

أُولَـٰئِكَ لَمْ يَكُونُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ۘ يُضَاعَفُ لَهُمُ الْعَذَابُ ۚ مَا كَانُوا يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ﴿٢٠﴾

20. Hao hawakuwa na uwezo wa kukwepa (Adhabu ya Allaah) katika ardhi (lau Angelitaka Kuwaadhibu) na wasingepata walinzi badala ya Allaah. Hao watazidishiwa adhabu. Hawakuwa wakiweza kusikia na hawakuwa wakiona (haki).

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٢١﴾

21. Hao ndio wale waliokhasirika nafsi zao, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).

 

 

 

لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ﴿٢٢﴾

22. Hapana shaka kwamba wao huko Aakhirah ni wenye kukhasirika zaidi. 

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَخْبَتُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٣﴾

23. Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakanyenyekea kwa Rabb wao, hao ni watu wa Jannah, na humo wao watadumu.    

 

 

 

مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَىٰ وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ ۚ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٢٤﴾

24. Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu na kiziwi na mwenye kuona na kusikia. Je, wanalingana sawa kwa kufananishwa?[12] Basi je, hamkumbuki?

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢٥﴾

25. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh kwa kaumu yake (akawaambia): Hakika mimi ni mwonyaji bayana kwenu.

 

 

 

أَن لَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٢٦﴾

26. Ya kwamba msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku inayoumiza.

 

 

 

فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا نَرَاكَ إِلَّا بَشَرًا مِّثْلَنَا وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَاذِبِينَ﴿٢٧﴾

27. Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: Hatukuoni isipokuwa ni mtu tu kama sisi, na hatukuoni wanaokufuata isipokuwa wale ambao ni duni wetu, wasiopevuka kifikra, na hatukuoneni kuwa mna chochote bora cha kutuzidi sisi, bali tuna yakini nyinyi ni waongo.

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي رَحْمَةً مِّنْ عِندِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمْ لَهَا كَارِهُونَ﴿٢٨﴾

28. (Nuwh) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na Amenipa Rehma (ya Unabiy na Risala) kutoka Kwake kisha ikakufichikieni, je, tukulazimisheni kuikubali (Tawhiyd ya Allaah) na hali nyinyi mnaichukia?

 

 

 

وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۚ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ إِنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ﴿٢٩﴾

29. Na enyi kaumu yangu! Sikuombeni mali juu ya (Risala) hii. Sina ujira isipokuwa kwa Allaah. Nami sitowafukuza wale walioamini. Hakika wao ni wenye kukutana na Rabb wao, lakini mimi nakuoneni ni watu majahili.

 

 

 

وَيَا قَوْمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِن طَرَدتُّهُمْ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣٠﴾

30. Na enyi kaumu yangu! Nani atakayeninusuru na Allaah nikiwafukuza? Je, hamkumbuki?

 

 

 

وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ وَلَا أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِي أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ اللَّـهُ خَيْرًا ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا فِي أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّي إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ﴿٣١﴾

31. Na wala sikuambieni kwamba mimi nina Hazina za Allaah, na wala sijui ya ghaibu, na wala sisemi mimi ni Malaika, na wala siwaambii wale ambao yanawadharau macho yenu kwamba Allaah Hatowapa kheri. Allaah Anajua zaidi yaliyomo katika nafsi zao. Hakika mimi hapo (nikifanya), bila shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

 

قَالُوا يَا نُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: Ee Nuwh, kwa yakini umelumbana nasi na umekithirisha malumbano nasi, basi tuletee hayo unayotuahidi ukiwa ni miongoni mwa wakweli.

 

 

قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُم بِهِ اللَّـهُ إِن شَاءَ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ﴿٣٣﴾

33. (Nuwh) akasema: Hakika hayo Atakuleteeni Allaah Akitaka, nanyi hamtaweza kushinda (kukwepa adhabu).

 

 

 

وَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ اللَّـهُ يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْ ۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٣٤﴾

34. Na wala haitokufaeni nasaha yangu nikitaka kukunasihini ikiwa Allaah Anataka kukuacheni mpotee. Yeye Ndiye Rabb wenu, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

 

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَعَلَيَّ إِجْرَامِي وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ﴿٣٥﴾

35. Bali wanasema ameitunga (Qur-aan). Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ikiwa nimeitunga, basi jarima hilo ni juu yangu, nami sina hatia ya jarima (zote) mnazofanya.

 

 

 

وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ﴿٣٦﴾

36.  Na Nuwh akafunuliwa Wahy kwamba: Hatoamini katika watu wako isipokuwa wale waliokwishaamini. Basi usisononeke kwa waliyokuwa wanayafanya.

 

 

 

وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚإِنَّهُم مُّغْرَقُونَ﴿٣٧﴾

37. Na unda jahazi mbele ya Macho Yetu[13] na kwa ufunuzi wa Wahy Wetu, na wala usinisemeze kuhusu wale waliodhulumu, hakika wao ni wenye kugharikishwa.

 

 

 

وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلَأٌ مِّن قَوْمِهِ سَخِرُوا مِنْهُ ۚ قَالَ إِن تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ﴿٣٨﴾

38. (Nuwh) akawa anaunda jahazi. Basi kila walipompitia wakuu katika kaumu yake walimfanyia dhihaka. Akasema: Ikiwa mnatufanyia dhihaka, basi nasi tutakufanyieni dhihaka kama vile mnavyotufanyia dhihaka.

 

 

 

فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٣٩﴾

39. Mtakuja kujua nani itakayemfikia adhabu itakayomhizi, na itakayemwangukia adhabu ya kudumu.

 

 

 

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٤٠﴾

40. Mpaka ilipokuja Amri Yetu na tanuri likafoka, Tukasema: Beba humo (jahazini) wawili wawili kutoka kila aina; dume na jike na ahli zako, isipokuwa (kafiri) ambaye imemtangulia kauli ya hukmu na (beba humo) wale walioamini. Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache.[14]

 

 

 

وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّـهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا ۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٤١﴾

41. Na (Nuwh) akasema: Pandeni humo! Kwa Jina la Allaah,[15] kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Rabb wangu bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ فِي مَعْزِلٍ يَا بُنَيَّ ارْكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ الْكَافِرِينَ﴿٤٢﴾

42. Basi hilo (jahazi) likawa linakwenda nao katikati ya mawimbi kama milima. Nuwh akamwita mwanawe naye alikuwa kandoni: Ee mwanangu! Panda pamoja nasi, na wala usiwe pamoja na makafiri.

 

 

 

قَالَ سَآوِي إِلَىٰ جَبَلٍ يَعْصِمُنِي مِنَ الْمَاءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ الْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚ وَحَالَ بَيْنَهُمَا الْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ الْمُغْرَقِينَ﴿٤٣﴾

43. Akasema: Nitakimbilia kwenye mlima utanilinda na maji. (Nuwh) akasema: Hapana wa kulindwa leo na Amri ya Allaah isipokuwa Aliyemrehemu. Tahamaki! Mawimbi yakaingia kati baina yao, akawa miongoni mwa waliogharikishwa.

 

 

 

وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ وَيَا سَمَاءُ أَقْلِعِي وَغِيضَ الْمَاءُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَاسْتَوَتْ عَلَى الْجُودِيِّ ۖ وَقِيلَ بُعْدًا لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿٤٤﴾

44. Na pakasemwa: Ee ardhi! Meza maji yako na ee mbingu, zuia (mvua), na maji yakadidimizwa, na hukmu ikatimizwa, na (jahazi) likatua juu ya (mlima wa) Judi.  Na pakasemwa: Wametokomelea mbali watu madhalimu!

 

 

 

وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ﴿٤٥﴾

45. Na Nuwh akamwita Rabb wake, akasema: Rabb wangu! Hakika mwanangu ni katika ahli zangu, na hakika Ahadi Yako ni ya kweli, Nawe Ni Mwadilifu zaidi wa kuhukumu kuliko mahakimu wote.

 

 

 

قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ ۖ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۖ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ﴿٤٦﴾

46. (Allaah) Akasema: Ee Nuwh! Hakika huyo si miongoni mwa ahli zako.[16] Hakika yeye amali zake si njema. Basi usiniombe yale usiyokuwa na ilimu nayo. Mimi Nakuwaidhi usijekuwa miongoni mwa majahili.

 

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ ۖ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴿٤٧﴾

47. Akasema: Ee Rabb wangu! Hakika mimi najikinga Kwako kukuomba yale nisiyo na ilimu nayo. Na Usiponighufuria na Ukanirehemu, nitakuwa miongoni mwa waliokhasirika.

 

 

 

قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٨﴾

48.  Pakasemwa: Ee Nuwh!  Teremka (jahazini) kwa salama (na amani) kutoka Kwetu na baraka nyingi juu yako, na juu ya nyumati zilizo pamoja na wewe. Na nyumati Tutakazozistarehesha, kisha zitawagusa kutoka Kwetu adhabu iumizayo.

 

 

 

تِلْكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَا أَنتَ وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَـٰذَا ۖ فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٤٩﴾

49. Hizo ni katika khabari za ghaibu Tunazokufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hukuwa unazijua wewe wala watu wako kabla ya hii (Qur-aan). Basi vuta subira, hakika hatima (nzuri) ni kwa wenye taqwa.

 

 

 

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ﴿٥٠﴾

50. Na kwa kina ‘Aad (Tulimpeleka) ndugu yao Huwd. Akasema: Ee kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Nyinyi si chochote isipokuwa watungao uongo.

 

 

 

يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿٥١﴾

51. Enyi kaumu yangu! Sikuombeni ujira juu ya hii (Risala). Haukuwa ujira wangu isipokuwa kwa Yule Aliyeniumba. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا مُجْرِمِينَ﴿٥٢﴾

52. Na enyi kaumu yangu! Mwombeni maghfirah Rabb wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu, na wala msikengeuke mkawa wahalifu.

 

 

 

قَالُوا يَا هُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِي آلِهَتِنَا عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ﴿٥٣﴾

53. Wakasema: Ee Huwd!  Hukutuletea hoja bayana, nasi hatutoacha kamwe waabudiwa wetu kutokana na kauli yako, nasi hatutokuwa wenye kukuamini.

 

 

 

إِن نَّقُولُ إِلَّا اعْتَرَاكَ بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُوءٍ ۗ قَالَ إِنِّي أُشْهِدُ اللَّـهَ وَاشْهَدُوا أَنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾

54. Hatusemi ila kuwa baadhi ya waabudiwa wetu wamekusibu kwa uovu. (Huwd) akasema: Hakika mimi namshuhudisha Allaah, na shuhudieni kwamba mimi niko mbali na waabudiwa mnaowashirikisha.

 

 

 

مِن دُونِهِ ۖ فَكِيدُونِي جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ﴿٥٥﴾

55. Bila kumjumuisha Yeye (Allaah). Basi nifanyieni njama nyote kisha msinipe muhula.

 

 

 

إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللَّـهِ رَبِّي وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٦﴾

56. Hakika mimi nimetawakali kwa Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakuna kiumbe chochote kitembeacho isipokuwa Yeye (Allaah) Ni Mwenye Kukamata hatamu za paji lake (Kukipeleka Atakavyo Yeye). Hakika Rabb wangu Yuko juu ya njia iliyonyooka.[17]

 

 

 

فَإِن تَوَلَّوْا فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَيْكُمْ ۚ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّي قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُ شَيْئًا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ﴿٥٧﴾

57. Mkikengeuka, basi nimekwishakubalighishieni (Risala) niliyotumwa nayo kwenu. Na Rabb wangu Atarithisha watu wengineo wasiokuwa nyinyi, na wala hamtaweza kumdhuru chochote. Hakika Rabb wangu Ni Mwenye Kuhifadhi kila kitu.

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَنَجَّيْنَاهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ﴿٥٨﴾

58. Na ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Huwd na wale walioamini pamoja naye kwa Rehma itokayo Kwetu, na Tukawaokoa kutokana na adhabu ngumu.

 

 

 

وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿٥٩﴾

59. Na hao ni kina ‘Aad. Wamezikanusha kwa ushupavu Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) za Rabb wao, na wakawaasi Rusuli Wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.

 

 

 

وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ عَادًا كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّعَادٍ قَوْمِ هُودٍ﴿٦٠﴾

60. Na wakafuatishwa na laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Hakika kina ‘Aad walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina ‘Aad; kaumu ya Huwd.

 

 

 

وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ﴿٦١﴾

61. Na kwa Thamuwd (Tulimpeleka) ndugu yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni kutokana na ardhi, na Akakufanyieni makazi humo, basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu Yuko Karibu, Mwenye Kuitikia.

 

 

 

قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ﴿٦٢﴾

62. Wakasema: Ee Swaalih! Kwa yakini ulikuwa kwetu mwenye kutarajiwa (kheri) kabla ya haya. Je, unatukataza kuabudu wale wanaoabudiwa na baba zetu, na hakika sisi tumo katika shaka na wasiwasi katika unayotuitia.

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ﴿٦٣﴾

63. (Swaalih) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, Naye Amenipa Rehma (Unabii na Risala) kutoka Kwake, hivo nani atakayeninusuru nikimuasi? Basi hamnizidishii ila khasara.

 

 

 

وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ﴿٦٤﴾

64. Enyi kaumu yangu! Huyu ni Ngamia Jike wa Allaah, ni Aayah (Ishara, Muujiza, Dalili ya wazi) kwenu, basi mwacheni ale katika Ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu ikakupateni adhabu iliyo karibu.

 

 

 

فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ﴿٦٥﴾

65. Lakini wakamuua. (Swaalih) akasema: Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo.

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿٦٦﴾

66. Basi ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa Rehma kutoka Kwetu, na (kuwaokoa) kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Rabb wako Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.

 

 

 

وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾

67. Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).

 

 

 

كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾

68. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd.

 

 

 

وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ﴿٦٩﴾

69. Na kwa yakini walimjia Ibraahiym Wajumbe Wetu kwa bishara, wakasema: Salaam! (Naye) Akasema: Salaam.  Basi hakukawia ila alikuja na ndama aliyebanikwa.

 

 

 

فَلَمَّا رَأَىٰ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۚ قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ﴿٧٠﴾

70. Alipoona mikono yao haisogei kumla (ndama) aliwashangaa na ikamuingia khofu kutokana nao. Wakasema: Usiogope! Hakika Sisi Tumetumwa kwa kaumu ya Luutw.

 

 

 

وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴿٧١﴾

71. Na mkewe amesimama wima, akacheka. Tukambashiria Is-haaq na baada ya Is-haaq ni Ya’quwb.

 

 

 

قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٧٢﴾

72.  Akasema: Yatakuwaje haya jamani! Je, nitazaa na hali mimi ni mkongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu!

 

 

 

قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ ۖ رَحْمَتُ اللَّـهِ وَبَرَكَاتُهُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ ۚ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ﴿٧٣﴾

73. (Malaika) wakasema: Je, unastaajabia Amri ya Allaah? Rehma ya Allaah na Baraka Zake ziko juu yenu enyi ahli wa nyumba (ya Nabiy Ibraahiym). Hakika Yeye Ni Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa, Mwenye Utukufu kamili na Enzi.

 

 

 

فَلَمَّا ذَهَبَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ الرَّوْعُ وَجَاءَتْهُ الْبُشْرَىٰ يُجَادِلُنَا فِي قَوْمِ لُوطٍ﴿٧٤﴾

74. Kisha kiwewe cha tisho la moyo kilipomuondoka Ibraahiym, na habari njema akawa ameipata (alianza) kujadiliana Nasi kuhusu kaumu ya Luutw.

 

 

 

إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّاهٌ مُّنِيبٌ﴿٧٥﴾

75. Hakika Ibraahiym bila shaka ni mvumilivu sana, mnyenyekevu mno kwa Allaah, na mwingi wa kurejea Kwake.

 

 

 

يَا إِبْرَاهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۖ إِنَّهُ قَدْ جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَإِنَّهُمْ آتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ﴿٧٦﴾

76. (Malaika wakamwambia): ee Ibraahiym! Achilia mbali haya! Hakika imekwishakuja Amri ya Rabb wako, na hakika wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ﴿٧٧﴾

77. Na Wajumbe Wetu walipomjia Luutw, alisononeka kwa ajili yao na akawaonea dhiki, akasema: Hii ni siku ngumu!

 

 

 

وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ﴿٧٨﴾

78. Wakamjia kaumu yake haraka, na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Luutw) akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa ni mabinti zangu, wao wametwaharika kwenu (kuwaoa kihalali). Basi mcheni Allaah, na wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Je, hakuna miongoni mwenu mtu muongofu?

 

 

 

قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ﴿٧٩﴾

79. Wakasema: Kwa yakini umekwishajua kwamba hatuhitaji wala hatuna matamanio yoyote kwa mabinti zako na bila shaka wewe unajua tunalolitaka.

 

 

 

 

قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ﴿٨٠﴾

80. (Luutw) akasema: Lau ningelikuwa nina nguvu ya kuzuia shari yenu, au nikimbilie katika nguzo madhubuti.

 

 

 

قَالُوا يَا لُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوا إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا امْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ﴿٨١﴾

81. (Malaika) wakasema: Ee Luutw! Hakika sisi ni Wajumbe wa Rabb wako, hawatokufikia (kwa uovu). Basi toka usiku (huu) na ahli zako sehemu iliyobakia ya usiku, na wala asitazame nyuma yeyote miongoni mwenu, isipokuwa mke wako (atabaki nyuma), kwani yeye yatamsibu yatakayowasibu wao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, kwani asubuhi haiko karibu?

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ﴿٨٢﴾

82. Basi ilipokuja Amri Yetu, Tuliupindua (mji wao) juu chini, na Tukauteremshia mvua ya mawe ya udongo mgumu uliookwa motoni, yenye kuandamana.

 

 

 

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ﴿٨٣﴾

83. Yametiwa alama kutoka kwa Rabb wako. Na adhabu hiyo haiko mbali na madhalimu (mfano wao).

 

 

 

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ﴿٨٤﴾

84. Na kwa Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Na wala msipunguze kipimo na mizani. Hakika mimi nakuoneni mko katika kheri (na neema), na hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku yenye kuzingira.

 

 

 

وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ﴿٨٥﴾

85. Na enyi kaumu yangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu, na wala msipunje watu vitu vyao, na wala msifanye uovu katika ardhi mkawa mafisadi.

 

 

 

بَقِيَّتُ اللَّـهِ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ﴿٨٦﴾

86. Mabakisho ya Allaah (Aliyokuwekeeni) ni bora kwenu, mkiwa ni wenye kuamini. Nami si mlinzi wa kuwachungeni.

 

 

 

قَالُوا يَا شُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ الْحَلِيمُ الرَّشِيدُ﴿٨٧﴾

87. Wakasema: Ee Shu’ayb! Hivi Swalaah zako ndizo zinakuamrisha kuwa sisi tuache yale baba zetu wanayoyaabudu, au tuache kufanya tunavyotaka katika mali zetu? Wewe kweli ni mvumilivu, uliyeongoka.

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ﴿٨٨﴾

88. (Shu’ayb) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, Naye Ameniruzuku riziki nzuri toka Kwake. Nami sitaki kukukhalifuni kufanya ninayokukatazeni. Sitaki lolote ila kutengeneza niwezavyo. Na sipati Tawfiyq ila kwa Allaah. Kwake natawakali na Kwake narejea kutubu.

 

 

 

وَيَا قَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَن يُصِيبَكُم مِّثْلُ مَا أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ ۚ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِّنكُم بِبَعِيدٍ﴿٨٩﴾

89. Enyi kaumu yangu! Kupingana nami kwa uhasama kusikuchocheeni kabisa yakakusibuni yale yaliyowasibu kaumu ya Nuwh au kaumu ya Huwd, au watu ya Swaalih. Na kaumu ya Luutw hawako mbali nanyi.

 

 

 

وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ﴿٩٠﴾

90. Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye Kurehemu, Mwenye upendo khalisi.

 

 

 

قَالُوا يَا شُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ﴿٩١﴾

91. Wakasema: Ee Shu’ayb! Hatufahamu mengi unayoyasema, na hakika sisi tunakuona ni dhaifu kati yetu. Na lau kama si (kabila au) jamaa zako tungelikupiga mawe. Nawe si azizi kwetu.

 

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ﴿٩٢﴾

92. (Shu’ayb) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, jamaa zangu wana utukufu zaidi kwenu kuliko Allaah, na mmemuweka Yeye (Allaah) nyuma ya migongo yenu? Hakika Rabb wangu ni Mwenye Kuyazunguka yale myatendayo.

 

 

 

وَيَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ ۖ وَارْتَقِبُوا إِنِّي مَعَكُمْ رَقِيبٌ﴿٩٣﴾

93. Na enyi kaumu yangu! Fanyeni kwa namna zenu, nami pia nafanya.  Mtakuja kujua nani itamfika adhabu itakayomhizi, na ni nani aliye muongo. Na ngojeeni mchunge. Hakika mimi niko pamoja nanyi nikingojea na kuchunga.

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٩٤﴾

94. Na ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa Rehma itokayo Kwetu. Na ukawachukuwa wale waliodhulumu ukelele angamizi wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).

 

 

 

كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ﴿٩٥﴾

95. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Watokomee mbali (watu wa) Madyan kama walivyotokomea Thamuwd.

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿٩٦﴾

96. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa kwa Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu na hoja bayana.

 

 

 

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ﴿٩٧﴾

97. Kwa Firawni na wakuu wake, lakini walifuata amri ya Firawni. Na amri ya Firawni haikuwa yenye uongofu.

 

 

 

يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ﴿٩٨﴾

98. (Firawni) atawatangulia watu wake Siku ya Qiyaamah, na atawafikisha motoni. Na ubaya ulioje mahali pa maingio watakapoingizwa!  

 

 

 

وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ﴿٩٩﴾

99. Na wamefuatishwa na laana katika (dunia) hii na Siku ya Qiyaamah (pia). Ubaya ulioje wa watakayotunukiwa (laana ya dunia na ya Aakhirah)!

 

 

 

ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْقُرَىٰ نَقُصُّهُ عَلَيْكَ ۖ مِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ﴿١٠٠﴾

100. Hizo ni baadhi ya khabari za miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), miongoni mwake ingalipo bado, na iliyofekwa.

 

 

 

وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ۖ فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ لَّمَّا جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ﴿١٠١﴾

101. Nasi Hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu nafsi zao wenyewe. Basi hawakuwafaa kitu chochote waabudiwa wao waliokuwa wakiwaomba badala ya Allaah ilipokuja Amri ya Rabb wako. Na wala hawakuwazidishia isipokuwa mateketezo.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾

102. Na hivyo ndivyo Mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika Mkamato Wake unaumiza vikali.

 

 

 

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ﴿١٠٣﴾

103. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara, Mazingatio) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.

 

 

 

وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ﴿١٠٤﴾

104. Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda maalumu unaohesabiwa. 

 

 

 

يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ﴿١٠٥﴾

105. Siku itakapofika, haitosema nafsi yeyote isipokuwa kwa Idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao watakuwa wenye mashaka na wenye furaha na neema.

 

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾

106. Ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni kupumua kwa mngurumo na kuvuta pumzi kwa mkoromo.

 

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ﴿١٠٧﴾

107. Watadumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Hakika Rabb wako Anafanya Atakavyo.

 

 

 

وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ﴿١٠٨﴾

108. Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, watadumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Ni hiba isiyokatizwa.

 

 

 

فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰؤُلَاءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنقُوصٍ﴿١٠٩﴾

109. Basi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) usiwe katika shaka kutokana na wanayoyaabudu hao (washirikina). Hawaabudu ila kama walivyoabudu baba zao kabla. Na hakika Tutawalipa kikamilifu fungu lao bila ya kupunguzwa.

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴿١١٠﴾

110. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu, zikatiwa ikhtilaafu ndani yake. Na kama si Neno lililotangulia kutoka kwa Rabb wako, bila shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wako katika shaka juu yake (hii Qur-aan) inayowatia wasiwasi.

 

 

 

وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚ إِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١١﴾

111. Na hakika wote Rabb wako Atawalipa kikamilifu amali zao. Hakika Yeye kwa yale wayatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿١١٢﴾

112. Basi thibitika imara kama ulivyoamrishwa wewe na aliyetubia pamoja nawe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye Ni Mwenye Kuona myatendayo.

 

 

 

وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ﴿١١٣﴾

113. Na wala msielemee kwa wale waliodhulumu usije ukakuguseni moto, na hamtokuwa na walinzi badala ya Allaah, kisha hamtonusuriwa.

 

 

 

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾

114. Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu.[18] Haya ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.[19]

 

 

 

وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١١٥﴾

115. Na vuta subira kwani hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.

 

 

 

فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ﴿١١٦﴾

116. Basi kwa nini hawakuweko katika karne za kabla yenu, walio weledi na wasaa wanakataza ufisadi katika ardhi isipokuwa wachache kati ya Tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu wakafuata anasa walizostareheshwa nazo na wakawa wahalifu.

 

 

 

وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ﴿١١٧﴾

117. Na Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza miji kwa dhulma na hali watu wake ni wenye kupigania mema.

 

 

 

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ﴿١١٨﴾

118. Na kama Angetaka Rabb wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja. Na hawatoacha kukhitilafiana.

 

 

 

إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ﴿١١٩﴾

119. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Rabb wako. Na kwa hayo ndio Amewaumba. Na limetimia Neno la Rabb wako (kwamba): Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu wote pamoja.

 

 

 

وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ ۚ وَجَاءَكَ فِي هَـٰذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿١٢٠﴾

120.  Na yote Tunayokusimulia katika khabari muhimu za Rusuli, ni ambayo kwayo Tunathibitisha moyo wako. Na imekujia katika haya haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.

 

 

 

وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَامِلُونَ﴿١٢١﴾

121. Na waambie wale wasioamini: Fanyeni kwa namna zenu, nasi pia tunafanya.

 

 

 

وَانتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ﴿١٢٢﴾

122. Na ngojeeni, nasi pia tunangojea.

 

 

 

وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴿١٢٣﴾

123. Na ni ya Allaah (Pekee) ghaibu ya mbingu na ardhi, na Kwake hurudishwa mambo yote, basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. Na Rabb wako Si Mwenye Kughafilika na yale myatendayo.

 

 

 

 

 

[1] الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).

 

[2] Umuhimu Na Faida Za Istighfaar (Kuomba Maghfirah) Na Kutubia Kwa Allaah (عزّ وجلّ):

 

Katika Suwrah hii Tukufu, Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja fadhila za Istighfaar (kuomba maghfirah) na kutubia katika Aayah kadhaa kama ifuatavyo:

 

(i) Kupata starehe nzuri. (ii) Kupewa Fadhila za Allaah (عزّ وجلّ), rejea Huwd (11:3). (iii) Kuteremshiwa mvua nyingi na kuzidishiwa nguvu, rejea Huwd (11:52). (iv) Kufanyiwa makazi. (v) Allaah Huwa Karibu na kuwaitikia duaa zao, rejea Huwd (11:61). (vi) Allaah Huwarehemu na Kuwa Mwenye Upendo Halisi kwao, rejea Huwd (11:90).  Na katika Suwrah nyenginezo mbalimbali, zimetajwa fadhila kama hizi na nyenginezo za kuomba maghfirah na kutubia. Rejea Suwrah Nuwh (71:10-12), na pia Aal-‘Imraan (3:125-136) ambamo kumetajwa fadhila ya kuingizwa Jannah. Hali kadhaalika, fadhila ya kuwekewa Nuru katika Swiraatw Siku ya Qiyaamah ambayo itammulikia mtu atakapokuwa akiivuka hiyo njia nyembamba mno kama unywele, rejea At-Tahriym (66:8). Pia ni mmojawapo ya sifa za Waja wa Ar-Rahmaan, rejea Al-Furqaan (25:70:71). Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja katika Qur-aan kuwa Anawapenda wenye kuomba maghfirah na tawbah, rejea Al-Baqarah (2:222).

 

Na kuomba maghfirah ni katika nyakati zozote zile, ila Allaah (سبحانه وتعالى) Amezitaja nyakati zilizo bora zaidi ambazo Anawasifu waja wema wanaoomba maghfirah katika nyakati hizo. Nyakati hizo ni za kabla ya Alfajiri, na Anawaahidi waja hao kuwaingiza Jannah. Rejea Adh-Dhaariyaat (51:15-18), Aal-‘Imraan (3:17). Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amehimizia waja kuomba maghfirah katika Hadiyth mbalimbali na akaonyesha mfano wake yeye kuwa anaomba maghfirah mara mia kwa siku moja kwa kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Enyi watu! Tubieni kwa Allaah na muombe maghfirah, kwani mimi natubia kwa Allaah na namuomba maghfirah mara mia kwa siku.” [Muslim]

 

Na fadhila za kuomba maghfirah katika Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni nyingi mno, bali Allaah Anafurahiwa mno na wenye kuomba maghfirah hata kwa mja aliyemkosea Allaah (سبحانه وتعالى) katika kumtaja Kwake! 

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Allaah Hufurahikiwa mno na tawbah ya mja Wake wakati anapotubia Kwake kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa amempanda mnyama wake kwenye jangwa (la joto kali, hakuna mtu yeyote), kisha mnyama huyo aliyebeba chakula chake na maji yake akampotea, na akakata tamaa kabisa ya kumpata tena. Akaenda kwenye mti, akalala chali ya kivuli chake huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpata tena mnyama wake. Akiwa katika hali hiyo (ya kutojua nini la kufanya), mara anashtuka kumwona huyo amesimama mbele yake, akaikamata hatamu yake, na kwa ile furaha akasema:  "Ee Allaah, Wewe ni mja wangu na mimi ni Rabb wako.” Alikosea (kumshukuru Rabb wake) kwa wingi wa furaha aliyokuwa nayo.” [Muslim]

 

Na Hadiyth Al-Qudsiy ifuatayo inaonyesha kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Hajali Mja Wake kuwa na madhambi madamu anamuomba maghfirah na tawbah:

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه):  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Allaah (تبارك وتعالى) Amesema: Ee binaadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali. Ee binaadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee binaadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana Nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]

 

Rejea An-Nisaa (4:110), Nuwh (71:10), Adh-Dhaariyaat (51:18), na At-Tahriym (66:8) ambako kumetajwa Tawbah ya kikweli na sharti za maghfirah na tawbah.

 

 

[3] Sababu Ya Makafiri Kuinamisha Vifua Vyao:

 

Makafiri walikuwa wakiinamisha vifua vyao kwa sababu wakimstahi Allaah (سبحانه وتعالى). Hadiyth ifuatayo imethibiti:

 

Amesimulia Muhammad Bin ‘Abaada Bin Ja’far (رضي الله عنه): ‘Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisoma:

أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ  

“Tanabahi! Hakika wao wanainamisha vifua vyao.” [Huwd (11:5)]

Nikamuuliza: Ee Ibn ‘Abbaas! Inamaanisha nini wanainamisha vifua vyao? Akasema: Mtu alikuwa akistahi kujamiiana na mkewe (katika sehemu iliyo wazi ili wasiwe ni wenye kuiona mbingu) au mtu alipokuwa akienda kufanya haja) basi Aayah hii iliteremshwa: 

أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ  

“Tanabahi! Hakika wao wanainamisha vifua vyao.”

 

Na pia Aayah inaendelea kutaja ada za makafiri kuweka vidole masikioni mwao na kujigubika nguo wasisikie Risala wala wasiwaone Rusuli wanaowalingania. Rejea Nuwh (71:7).

 

[5]Arshi ya Allaah Kuwa Juu Ya Maji:

 

Aayah hii tukufu inataja kuwa ‘Arshi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumba mbingu na ardhi. Na ‘Arshi hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى) na hayo maji ni vitu Alivyoviumba Allaah (عزّ وجلّ) na ambavyo Amevinasibisha Kwake Mwenyewe Allaah عزّ وجلّ)), hatuvijui uhakika wake, bali tunaamini kama Anavyosema. Rejea Twaahaa (10:5). Na baadhi ya Hadiyth zifuatazo zinathibitisha na zinatilia nguvu Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) ya Aayah hii tukufu kuhusu ‘Arsh Yake Allaah (عزّ وجلّ) kuwa ilikuwa juu ya maji:

 

Amesimulia ‘Imraan Bin Huswayn (رضي الله عنه): Nilikwenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumfunga ngamia wangu jike mlangoni. Watu wa Bani Tamiym walikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Enyi Bani Tamiym! Pokeeni bishara njema.” Wakasema mara mbili: “Umetupatia bishara njema, sasa tupatie kitu.” Kisha baadhi ya watu wa Yemen walikuja kwake, akasema: “Pokeeni bishara njema, enyi watu wa Yemen, kwani Bani Tamiym wamekataa.” Wakasema: “Tunaipokea ee Rasuli wa Allaah! Tumekuja kukuuliza kuhusu jambo hili (yaani mwanzo wa uumbaji).” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Kwanza kabisa, hapakuwa na chochote ila Allaah (kisha Akaumba ‘Arshi Yake). ‘Arshi Yake ilikuwa juu ya maji, na Akaandika kila kitu katika Kitabu (cha mbinguni) na Akaumba mbingu na ardhi." Akanadi mtu mmoja kwa sauti: “Ee Ibn Huswayn! Ngamia wako jike amekimbia!” Nikaondoka mbio, lakini sikuweza kumuona ngamia wangu jike kwa sababu ya mazigazi. Naapa kwa Allaah! Natamani ningekuwa nimemuachilia mbali ngamia huyo jike (na sio kuacha kikao hicho).  [Al-Bukhaariy]

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Aliandika (kwenye Al-Lawh Al-Mahfuwdh) makadirio na hatima ya viumbe wote kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu khamsini, na 'Arsh Yake ilikuwa juu ya maji."  [Muslim]

 

Na pia, Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mkono wa Allaah Umejaa (pomoni) na (kujaa kwake) hakuathiriki kwa kutoa mfululizo usiku na mchana.” Na Akasema tena: “Je, hamuoni kwa Alivyotoa kuanzia Alipoumba mbingu na ardhi? Hata hivyo, vilivyo mkononi Mwake havijapungua.” Na akasema tena: “Arshi Yake ipo juu ya maji, na katika Mkono Wake mwengine kuna Mizani (ya uadilifu), kwayo Hunyanyua (watu wengine) na kuwateremsha (wengine).” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]

 

[6] Maana Mojawapo Ya أُمَّة Ni Muda: 

 

Rejea An-Nahl (16:120) kwenye maelezo bayana.

 

[7] Hali Ya Makafiri Na Waumini Katika Kupatwa Dhara Na Kuondoshewa Neema:

 

Aayah hii ya Huwd (11:9), inyofuatia (11:10), inataja hali ya makafiri ambao hawana subira wanapopatwa na dhara au mitihani, au wanapoondoshewa Rehma na Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), wala hawana shukurani kwa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kila hali. Ama Waumini wanapofikwa na dhara au mitihani, wao ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah inayofuatia ya Huwd (11:10) kwamba wao ni wenye kuvuta subira na kuendelea kuthibitia katika imaan zao wakaendelea kutenda mema. Basi Waumini hao ni kama walivyosifiwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ajabu ya hali ya Muumini kuwa mambo yake yote ni kheri; anapofikwa na furaha hushukuru na huwa kheri kwake, na anapofikwa na matatizo husubiri na huwa ni kheri kwake, na haiwi hivyo (sifa hiyo) ila kwa Muumini.”[Muslim]

 

Rejea pia Yuwnus (10:12), Az-Zumar (39:49), Ar-Ruwm (30: 33).

 

[8] Hali Ya Binaadam Asiyekuwa Muumini Anapopatwa Dhara:

 

Rejea Yuwnus (10:12).

 

[9] Changamoto Makafiri Walete Mfano Wa Qur-aan Lakini Kamwe Hawatoweza!

 

Rejea Yuwnus (10:38), Al-Israa (17:88), Al-Baqarah (2:23-24), Atw-Twuwr (52:33-34). Rejea pia Al-An’aam (6:93) ambako kumetajwa waongo waliodai Unabii.

 

[10] Wanaopendelea Dunia Badala Ya Aakhirah:

 

Rejea Ash-Shuwraa (42:20).

 

[11] Shahidi: Ni Jibriyl Au Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Tawraat:

 

Je yule aliyekuwa kwenye hoja na baswiyrah (dalili bayana, ujuzi, umaizi) kutoka kwa Rabb wake katika kile anachokiamini na anachokilingania kwa Wahy ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Ameuteremsha ushahidi huu, ukafuatiwa na hoja nyengine kutoka Kwake yenye kuutolea ushahidi; naye ni Jibril au ni Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na ukatiliwa nguvu, na dalili ya tatu kabla ya Qur-aan, nayo ni Tawraat kitabu alichoteremshiwa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام)  chenye uongozi na Rehma kwa waliokiamini, basi (je yeye) ni kama yule ambaye hima yake ilikuwa ni maisha yenye mapambo na ya kutoweka? Hao wanaiamini hii Qur-aan, wanazifuata hukmu zake kivitendo. Na mwenye kuikanusha hii Qur-aan miongoni mwa wale waliojikusanya kumpinga Rasuli  wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi jazaa yake ni moto, hapana budi atauingia. Basi [ee Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)] usiwe na shaka juu ya Qur-aan kwamba inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya dalili na hoja kuitolea ushahidi. Na ujue kwamba Dini hii ndio ya haki na ya ukweli unaotoka kwa Rabb wako, lakini wengi wa watu hawaamini wala hawayatendi yale wanayoamrishwa. Huu ni mwongozo jumuishi kwa Ummah wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[12] Mifano Ya Tofauti Ya Kafiri Na Muumini:

 

Rejea Al-an’aam (6:122), Faatwir (35:19).

 

[13] Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Tawqiyfiyyah Na Hii Ndio ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah:

 

Macho ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni Sifa inayopaswa kuthibitishwa hivyo hivyo kama Anavyoitaja Mwenyewe bila ya Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).

 

Hivyo basi Anaposema kuwa Anayo Macho, sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Macho. Na Anaposema kuwa Ana Masikio, sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Masikio. Anaposema kuwa Anayo Mikono, sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Mikono, na Anaposema kuwa Anayo Nafsi, na sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Nafsi. Na Anaposema kuwa Anao Wajihi, sisi ni lazima tuamini kuwa Anao Wajihi. Lakini Macho Yake au Masikio Yake au Mikono Yake, Au Nafsi Yake, au Wajihi Wake, hakuna kabisa mfano Wake kwa kiumbe chochote kile kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى): 

 

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.” [Ash-Shuwraa (42:11)]

 

Rejea zifuatazo zinataja baadhi ya Sifa Zake: Nafsi Yake: Aal-‘Imraan (3:28), Al-An’aam (6:12), (6:54), Wajihi Wake: Al-Qaswasw (28:88), Al-Baqarah (2:115) na Ar-Rahmaan (55:27). Mkono au Mikono Yake: Swaad (38:75), Al-Fat-h (48:10). Macho Yake: Suwrah hii ya Huwd (11:37), Al-Muuminuwn (23:27), Twaahaa (20:39). Kusikia na Kuona Kwake:  Twaahaa (20:46).

 

[14] Nabiy Nuwh (عليه السّلام) Na Kizazi Kilobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):

 

Ijtihaad za Mufassiruwn wamesema kuwa watu walioamini wakapanda jahazini, walikuwa ni themanini.  Miongoni mwao, walikuwa watoto watatu wa Nabiy Nuwh (عليه السّلام) ambao ni Saam, Haam na Yaafith. Na pia walikuwemo wake zao. Wengine wanasema walikuwa watu sabini na mbili, na wengine wamesema ni watu kumi.

 

Ibn ‘Abbaas amesema walikuwa watu themanini wakiwemo wanawake wao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Basi hao ndio walioeneza tena kizazi cha wanaadam mpaka tukapatikana sisi na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا ﴿٣﴾

“Enyi kizazi cha ambao Tuliwabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi). Hakika yeye alikuwa mja mwingi wa shukurani.”  [Al-Israa (17:3)]

 

Rejea Asw-Swaaffaat (37:77) kwenye maelezo bayana na rejea zake mbalimbali.

 

Rejea Yuwnus (10:73), Maryam (19:58), Al-Muuminuwn (23:27), Nuwh (71:1).

 

 

[15] Kutaja Jina La Allaah Katika Kupanda Chombo:

 

Muislamu anapopanda chombo chochote anatakiwa kuanza kwa بِسْمِ اللَّـهِ  . Na pia kuna duaa ya kupanda kipando, rejea Az-Zukhruf (43:13-14), na pia  Al-Muuminuwn (23:28-28).

 

[16] Nabii Ambao Ahli Zao Walikuwa Makafiri:

 

Baadhi ya Nabii walikuwa na ahli zao ambao hawakuamini, bali walikanusha Risala, au walikuwa katika maasi, nao ni:

 

Nabiy Nuwh: Mwanawe kama ilivyotajwa katika Aayah hizi (11:42-47), na mkewe. Rejea Suwrah hii Aayah (11:40), kwani waliokusudiwa katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):   

إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ  

“Isipokuwa (kafiri) ambaye imemtangulia kauli ya hukmu.”

 

Ni mke wa Nuhw ambaye hakuamini. [Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Nabiy Luutw: Rejea Suwrah hii Huwd (11:81), Al-Hijr (15:60), na Al-‘Ankabuwt  (29: 33).

 

Nabiy Ibraahiym: Baba yake Aazar. Rejea Al-An’aam (6:74), na At-Tawbah (9:114).

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): ‘Amm yake Abu Twaalib. Alijaribu kumlingania katika Uislamu lakini alikataa, akafariki akiwa ni kafiri. Rejea Al-Qaswasw (28:56).

 

Hivyo basi, uhusiano wa undugu wa Kiislamu, ni undugu ulio na nguvu, imaan na mapenzi kulikoni uhusiano wa damu wa makafiri, na ndio maana Allaah (سبحانه وتعالى)  Anasema: Waumini ni ndugu. Rejea Al-Hujuraat (49:10).

 

[17]  Maana Ya: Rabbi Yuko Juu Ya Njia Iliyonyooka:

 

Maana ya:

إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٦﴾

“Hakika Rabb wangu Yuko juu ya njia iliyonyooka.” [Huwd (11:56)]

 

Ina maana: Ana uadilifu, Ana Hikmah, Ana Himdi katika Qadhwaa na Qadar (Yaliyohukumiwa na Yaliyokadiriwa), katika Sharia Zake na Amri Zake, katika Jazaa (Malipo) Yake na Thawabu Zake, na Adhabu Zake, Matendo Yake hayaondoki kwenye Njia Iliyonyooka, ambayo Inahimidiwa Na Kutukuzwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[18] Swalaah Inafuta Madhambi Na Mema Yanaondosha Maovu:

 

Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesimulia: Mwanamume mmoja alimbusu mwanamke (kinyume na sharia) kisha akaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumhadithia. Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

 وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾

“Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu. Haya ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.” [Huwd (11:114)] 

 

Yule mtu akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Je, hii (Aayah) ni kwa ajili yangu tu? Akajibu: “Ni kwa ajili ya watakaoitendea kazi katika ummah wangu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

Pia Hadiyth nyenginezo kadhaa zimetaja kuhusu Muislamu anapotenda mema Allaah (سبحانه وتعالى) Humfutia makosa au madhambi yake, baadhi yake ni zifuatazo:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mnaonaje ingelikuwa kuna mto mbele ya nyumba ya mmoja wenu kisha akawa anaoga humo kila siku mara tano, je atabakiwa na uchafu?” Wakasema: “Habakiwi na uchafu.” Akasema: “Hivyo ni mfano wa Swalaah ambazo Allaah hufuta madhambi kwazo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Amesimulia ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayetawadha kwa ajili ya Swalaah, akafanya vizuri wudhuu wake, kisha akaenda kuswali Swalaah za fardhi, akaziswali pamoja na watu au jamaa au Msikitini, basi Allaah Atamfutia madhambi yake.” [Muslim]

 

Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Swalaah tano, na Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhwaan hadi Ramadhwaan, zinafuta madhambi baina yake pindi madhambi makubwa yakiepukwa.”  [Muslim]

 

Rejea pia Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى): Al-Furqaan (25:70), Al-Maaidah (5:65), Ar-Ra’d (13:22), Fusswilat (41:24), na Al-Muuminuwn (23:96).

 

Share