028 - Al-Qaswasw

 

  الْقَصَص

 

028-Al-Qaswasw

 

 

028-Al-Qaswasw: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com  

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

طسم ﴿١﴾

1. Twaa Siyn Miym.[1]

 

 

 

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2.  Hizi ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.

 

 

 

نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣﴾

3. Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari za Muwsaa na Firawni kwa haki kwa watu wanaoamini.

 

 

 

 

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٤﴾

4. Hakika Firawni alitakabari katika ardhi, na akawafanya watu wake makundi mbali mbali, akikandamiza kundi miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiacha hai wanawake wao. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa mafisadi.

 

 

 

وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴿٥﴾

5. Na Tukataka Tuwafanyie fadhila wale waliokandamizwa katika ardhi, na Tuwafanye viongozi na Tuwafanye wenye kurithi.

 

 

 

 

وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ ﴿٦﴾

6. Na Tuwamakinishe kwa uwezo katika ardhi, na Tumwonyeshe Firawni na Haamaan na majeshi yao miongoni mwao yale waliyokuwa wakitahadhari.

 

 

 

 

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾

7. Na Tukamtia ilhamu mama yake Muwsaa kwamba: Mnyonyeshe. Lakini utakapomkhofia, basi mtupe katika mto na wala usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi Tutamrudisha kwako, na Tutamfanya miongoni mwa Rusuli.

 

 

 

 

فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا ۗ إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ ﴿٨﴾

8. Basi wakamwokota watu wa Firawni ili awe adui kwao na (sababu ya) huzuni. Hakika Firawni na Haamaan na majeshi yao walikuwa wenye makosa.

 

 

 

وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. Na mke wa Firawni akasema: Kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Usimuue, asaa akatufaa au tumfanye mwana. Nao hawatambui.

 

 

 

 

وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠﴾

10. Na ukawa moyo wa hisia na mwazo wa mama yake Muwsaa mtupu! Alikaribia kumdhihirisha (kuwa ni mwanawe) lau kama Tusingeutia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.

 

 

 

 

وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ ۖ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١١﴾

11. Akamwambia ukhti wake (Muwsaa): Mfuatilie!  Akamtazama kwa mbali nao hawatambui.

 

 

 

 

وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ ﴿١٢﴾

12. Na Tulimharamishia akatae kabisa wanyonyeshaji tangu mwanzo. Kisha (ukhti wake Muwsaa) akasema: Je, nikuelekezeni kwa watu wa nyumba watakaomlea kwa ajili yenu, nao watakuwa wenye kumweka vyema kidhati?

 

 

 

فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Basi Tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake na wala asihuzunike, na ili ajue kwamba Ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawajui.

 

 

 

 

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤﴾

14. Na alipofikia umri wa kupevuka na akaimarika sawasawa, Tulimpa hikmah na ilimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

 

وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ قَالَ هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّهُ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. Na akaingia mjini wakati watu wake wako katika mighafiliko, akakuta humo watu wawili wanapigana; mmoja ni miongoni mwa kundi lake, na mwengine ni miongoni mwa adui zake. Yule ambaye ni katika kundi lake akamuomba ukozi[2] dhidi ya yule ambaye ni adui yake. Muwsaa akampiga ngumi, akamuua. Akasema: Hii ni kutokana na kitendo cha shaytwaan. Hakika yeye ni adui mpotoaji bayana.

 

 

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٦﴾

16. Akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie. Akamghufuria. Hakika Yeye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ ﴿١٧﴾

17. Akasema: Rabb wangu! Kwa Uliyonineemesha, sitokuwa kamwe msaidizi kwa wahalifu.

 

 

 

 

فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ ۚ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٨﴾

18. Akapambaukiwa kuwa mwenye khofu katika mji ule anaangaza kwa tahadhari. Basi mara yule aliyemuomba amnusuru jana anampigia kelele amsaidie. Muwsaa akamwambia: Hakika wewe ni mpotofu bayana.

 

 

 

 

فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِ ۖ إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٩﴾

19. Na alipotaka kumpa kipigo cha nguvu yule aliye adui wao wote wawili, alisema: Ee Muwsaa! Je, unataka kuniua kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki lolote isipokuwa unataka uwe jabari katika nchi, na wala hutaki kuwa miongoni mwa wasuluhishaji.

 

 

 

 

وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾

20. Akaja mtu kutoka mwisho wa mji ule akiwa anakimbia, akasema: Ee Muwsaa!  Hakika wakuu wanashauriana dhidi yako ili wakuue! Basi toka, hakika mimi ni miongoni mwa wanaokunasihi.

 

 

 

 

فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ ۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢١﴾

21. Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari. Akasema: Rabb wangu! Niokoe na watu madhalimu.

 

 

 

 

وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿٢٢﴾

22. Na alipoelekea upande wa Madyan, akasema: Asaa Rabb wangu Akaniongoza njia iliyo sawa.

 

 

 

 

وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ ﴿٢٣﴾

23. Alipofikia maji ya Madyan, alikuta kundi la watu linanywesha maji (wanyama wao), na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana.

 

 

 

 

فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾

24. Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: Rabb wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia.[3] 

 

 

 

 

فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾

25. Akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kustahi, akasema: Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipomfikia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usikhofu, umeokoka na watu madhalimu.

 

 

 

 

قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴿٢٦﴾

26. Mmoja wao akasema: Ee baba yangu kipenzi!  Muajiri! Hakika mbora uwezaye kumwajiri ni mwenye nguvu mwaminifu.

 

 

 

 

 

قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾

27. Akasema: Mimi nataka nikuozeshe mmojawapo wa binti zangu hawa wawili kwa sharti kuwa unitumikie miaka minane. Ukitimiza kumi, basi ni uamuzi wako. Na wala sitaki kukutia mashakani. Utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

 

 

قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ ۖ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ ۖ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾

28. (Muwsaa) akasema: Hayo ni baina yangu na baina yako. Muda wowote kati ya miwili nitakaoutimiza basi hakuna uadui juu yangu. Na Allaah juu ya yale tunayoyasema ni Mdhamini.

 

 

 

 

فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٢٩﴾

29. Basi Muwsaa alipotimiza muda, na akasafiri pamoja na ahli zake, akaona aliona moto upande wa mlima. Akawaambia ahli zake: Bakieni, hakika mimi nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo khabari, au kijinga cha moto ili mpate kuota moto.

 

 

 

 

فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٠﴾

30. Basi alipoufikia, akaitwa kutoka upande wa kulia wa bonde katika sehemu iliyobarikiwa kutoka mtini kwamba: Ee Muwsaa! Hakika Mimi Ni Allaah, Rabb wa walimwengu.

 

 

 

 

وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ ۖ إِنَّكَ مِنَ الْآمِنِينَ ﴿٣١﴾

31. Na tupa fimbo yako! Basi alipoiona inataharuki kama kwamba ni nyoka, aligeuka kukimbia bila kutazama nyuma wala hakurudi. Ee Muwsaa! Njoo mbele, na wala usikhofu! Hakika wewe ni miongoni mwa waliokuwa katika amani.

 

 

 

 

اسْلُكْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ وَاضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ الرَّهْبِ ۖ فَذَانِكَ بُرْهَانَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٣٢﴾

32. Ingiza mkono wako kifuani katika uwazi wa nguo yako, utatoka kuwa mweupe (wenye kun’gara) bila ya dhara (magonjwa) yoyote. Na ambatisha mkono ubavuni mwako kujikinga na khofu. Hizo ni dalili mbili za wazi kutoka kwa Rabb wako kwa Firawni na wakuu wake. Hakika wao walikuwa watu mafasiki.

 

 

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿٣٣﴾

33. Akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimeua mtu miongoni mwao, na nakhofu wataniua.

 

 

 

 

وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءًا يُصَدِّقُنِي ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿٣٤﴾

34. Na kaka yangu Haaruwn yeye ana ufasaha zaidi wa lugha kuliko mimi, basi mpeleke pamoja nami, kama msaidizi wangu anisadikishe. Hakika mimi nakhofu watanikadhibisha.

 

 

 

 

قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَانًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا ۚ بِآيَاتِنَا أَنتُمَا وَمَنِ اتَّبَعَكُمَا الْغَالِبُونَ ﴿٣٥﴾

35. (Allaah) Akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na Tutakupeni madaraka, basi hawatakufikilieni. Kwa sababu ya Aayaat (Miujiza, Hoja, Dalili) Zetu, nyinyi wawili na watakaokufuateni mtashinda.

 

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ ﴿٣٦﴾

36. Basi Muwsaa alipowajia (kina Firawni) kwa Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu bayana, walisema: Hii si chochote isipokuwa ni sihiri iliyotungwa, na hatukusikia haya kwa baba zetu wa awali.

 

 

 

 

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِ وَمَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٣٧﴾

37. Muwsaa akasema: Rabb wangu Anajua zaidi yule ajaye na mwongozo kutoka Kwake, na yule atakayekuwa na hatima njema ya makazi ya Aakhirah. Hakika madhalimu hawafaulu.

 

 

 

 

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي فَأَوْقِدْ لِي يَا هَامَانُ عَلَى الطِّينِ فَاجْعَل لِّي صَرْحًا لَّعَلِّي أَطَّلِعُ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٣٨﴾

38. Firawni akasema: Enyi wakuu! Sijui kama mnaye mwabudiwa badala yangu. Basi niwashie moto ee Haamaan unichomee udongo, unifanyie mnara mrefu ili nimwangalie Ilaah wa Muwsaa, na hakika mimi bila shaka nina yakini yeye ni miongoni mwa waongo.

 

 

 

 

وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ ﴿٣٩﴾

39. (Firawni) akatakabari yeye na jeshi lake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kwamba wao Kwetu hawatorejeshwa.

 

 

 

 

فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٤٠﴾

40. Basi Tukamchukua na jeshi lake, Tukawatupilia mbali baharini. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya madhalimu.

 

 

 

 

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾

41. Na Tukawafanya viongozi wanaolingania motoni, na Siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa.

 

 

 

وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾

42. Na Tukawafuatishia laana katika dunia hii. Na Siku ya Qiyaamah wao ni miongoni mwa wenye kubaidishwa na Rehma (ya Allaah).

 

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ مِن بَعْدِ مَا أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ الْأُولَىٰ بَصَائِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu baada ya kuwa Tumeshaangamiza karne za awali kiwe ni kifumbuzi macho kwa watu, na mwongozo na rehma ili wakumbuke.  

 

 

 

 

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الْغَرْبِيِّ إِذْ قَضَيْنَا إِلَىٰ مُوسَى الْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٤٤﴾

44. Na wala hukuweko (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kando ya Magharibi (ya mlima) Tulipomkidhia Muwsaa amri, na wala hukuwa miongoni mwa walioshuhudia.

 

 

 

 

وَلَـٰكِنَّا أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِي أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَلَـٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ ﴿٤٥﴾

45. Lakini Sisi Tulianzisha karne nyingi ukawatawilikia umri. Na wala hukuwa mkaazi katika watu wa Madyan ukiwasomea Aayaat Zetu, lakini Sisi Tulikuwa Watumaji (Rusuli).

 

 

 

 

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَـٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٦﴾

46. Na wala hukuwa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kando ya mlima Tuliponadi, lakini ni rehma kutoka kwa Rabb wako ili uonye watu ambao hawakufikiwa na mwonyaji yeyote kabla yako ili wapate kukumbuka.

 

 

 

 

وَلَوْلَا أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾

47. Na usije ukawasibu msiba kwa yale iliyotanguliza mikono yao, wakasema: Rabb wetu! Kwa nini Hukututumia Rasuli tukafuata Aayaat Zako, na tuwe miongoni mwa Waumini.

 

 

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ مُوسَىٰ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ ﴿٤٨﴾

48. Basi ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: Mbona hakupewa mfano wa yale aliyopewa Muwsaa? Je, kwani hawakuyakufuru yale aliyopewa Muwsaa kabla? Wakasema: Sihri mbili (Tawraat na Qur-aan) zimesaidiana. Na wakasema: Hakika sisi kwa vyote viwili ni wenye kuvikanusha.

 

 

 

 

قُلْ فَأْتُوا بِكِتَابٍ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَا أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٩﴾

49. Sema: Leteni Kitabu kutoka kwa Allaah ambacho ni mwongozo zaidi kuliko hivyo viwili nikifuate, mkiwa ni wakweli.

 

 

 

 

فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٠﴾

50. Na wasipokuitikia basi juwa kwamba hakika wanafuata hawaa zao. Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata hawaa zake bila ya mwongozo kutoka kwa Allaah? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

 

 

وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥١﴾

51. Na kwa yakini Tumewafuatilishia na kuwateremshia sehemu kwa sehemu ya Neno ili wapate kukumbuka.[4]

 

 

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾

52. Wale Tuliowapa Kitabu kabla yake, wao wanaiamini (Qur-aan).[5]

 

 

 

 

وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾

53. Na wanaposomewa husema: Tumeiamini, hakika hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wetu, hakika Sisi kabla yake tulikuwa Waislamu (waliojisalimisha kwa Allaah).

 

 

 

أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾

54. Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa vile walivyosubiri, na wanazuia ubaya kwa wema, na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.

 

 

 

 

وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ وَقَالُوا لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِي الْجَاهِلِينَ ﴿٥٥﴾

55. Na wanaposikia maneno ya upuuzi hujitenga nayo, na husema: Sisi tuna amali zetu, nanyi mna amali zenu. Salaamun ‘alaykum! (Amani iwe juu yenu)!  Hatushindani na majahili.

 

 

 

 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

56. Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye, lakini Allaah Humhidi Amtakaye,[6] Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.

 

 

 

 

 

وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا ۚ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾

57. Wakasema: Tukifuata mwongozo pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka ardhi yetu. Je, kwani Hatukuwamakinisha mahali patukufu, na pa amani ambapo huletewa mazao ya kila kitu kuwa ni riziki kutoka Kwetu!   Lakini wengi wao hawajui.   

 

 

 

 

وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا ۖ فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na miji mingapi Tumeiangamiza!   Ilipinduka mno mipaka ya kukanusha haki na neema za maisha yake. Basi hayo ni masikani yao yasiyokaliwa baada yao isipokuwa kidogo tu. Na Tukawa Sisi Warithi.

 

 

 

 

وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِي أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۚ وَمَا كُنَّا مُهْلِكِي الْقُرَىٰ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَالِمُونَ ﴿٥٩﴾

59. Na Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza miji mpaka Apeleke katika miji mikuu yake Rasuli awasomee Aayaat Zetu. Na Hatukuwa Wenye Kuangamiza miji isipokuwa watu wake wawe madhalimu.

 

 

 

 

وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾

60. Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

 

أَفَمَن وَعَدْنَاهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَاقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَاهُ مَتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٦١﴾

61. Je, yule Tuliyemuahidi ahadi nzuri (Jannah) kisha yeye atakutana nayo, ni sawa na yule Tuliyemstarehesha starehe za uhai wa dunia, kisha yeye Siku ya Qiyaamah ni miongoni mwa watakaohudhurishwa? 

 

 

 

 

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٦٢﴾

62. Na Siku (Allaah) Atakayowaita, Atasema: Wako wapi hao mliokuwa mnadai kwa dhana kuwa ni washirika Wangu?

 

 

 

 

 

قَالَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَغْوَيْنَا أَغْوَيْنَاهُمْ كَمَا غَوَيْنَا ۖ تَبَرَّأْنَا إِلَيْكَ ۖ مَا كَانُوا إِيَّانَا يَعْبُدُونَ ﴿٦٣﴾

63. Watasema wale iliyowathibitikia kauli: Rabb wetu! Hawa ndio wale tuliowapotoa. Tumewapotoa kama tulivyopotoka. Tumejitoa hatiani mbele Yako, hawakuwa wakituabudu sisi.

 

 

 

 

وَقِيلَ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَرَأَوُا الْعَذَابَ ۚ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا يَهْتَدُونَ ﴿٦٤﴾

64. Na itasemwa: Iteni washirika wenu. Watawaita lakini hawatowaitikia, na wataiona adhabu, laiti wao wangelikuwa wamehidika.

 

 

 

 

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na Siku (Allaah) Atakapowaita, Atasema: Mliwajibu nini Rusuli?

 

 

 

 

فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿٦٦﴾

66. Basi zitawafichikia khabari Siku hiyo, nao hawatoweza kuulizana.

 

 

 

 

فَأَمَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَعَسَىٰ أَن يَكُونَ مِنَ الْمُفْلِحِينَ ﴿٦٧﴾

67. Ama yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema, basi asaa akawa miongoni mwa waliofaulu.

 

 

 

 

 

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾

68. Na Rabb wako Anaumba na Anachagua Atakavyo. Haikuwa wao wana khiari yoyote. Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha.

 

 

 

 

وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٦٩﴾

69. Na Rabb wako Anayajua yale yanayofichwa na vifua vyao, na yale   wanayoyafichua.

 

 

 

 

وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾

70. Naye ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Ni Zake Pekee Himidi za mwanzoni (duniani) na za Aakhirah. Na Hukumu ni Yake Pekee, na Kwake Pekee mtarejeshwa.

 

 

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِضِيَاءٍ ۖ أَفَلَا تَسْمَعُونَ ﴿٧١﴾

71. Sema: Je, mnaonaje kama Allaah Angelikufanyieni usiku unaendelea daima dawamu mpaka Siku ya Qiyaamah, nani mwabudiwa ghairi ya Allaah Atakayekuleteeni mwanga? Je, basi hamsikii?

 

 

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٧٢﴾

72. Sema: Je, mnaonaje kama Allaah Angelikufanyieni mchana unaendelea daima dawamu mpaka Siku ya Qiyaamah, nani mwabudiwa ghairi ya Allaah Atakayekuleteeni usiku mpate utulivu humo? Je, basi hamuoni?

 

 

 

 

وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾

73. Na kutokana na Rehma Yake, Amekufanyieni usiku na mchana ili mpate utulivu humo, na ili mpate kutafuta katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.

 

 

 

 

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٧٤﴾

74. Na Siku (Allaah) Atakayowaita, Atasema: Wako wapi hao mliokuwa mnadai kwa dhana kuwa ni washirika Wangu?

 

 

 

 

وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّـهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٧٥﴾

75. Na Tutachomoa toka kila ummah shahidi kisha Tutasema: Leteni ushahidi wenu wa wazi. Basi watajua kwamba haki ni ya Allaah Pekee, na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).

 

 

 

 

إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ ﴿٧٦﴾

76. Hakika Qaaruwn[7] alikuwa miongoni mwa kaumu ya Muwsaa, lakini aliwafanyia uonevu kwa kutakabari. Na Tulimpa hazina ambazo funguo zake zinalemea kundi la watu wenye nguvu (kuzibeba). Walipomwambia watu wake: Usifurahi kwa kujigamba. Hakika Allaah Hapendi wanaofurahi kwa kujigamba.

 

 

 

 

 

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّـهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٧٧﴾

77. Na tafuta katika yale Aliyokupa Allaah makazi ya Aakhirah. Na wala usisahau fungu lako katika dunia. Na fanya ihsaan kama Alivyokufanyia Allaah ihsaan, na wala usitake ufisadi ardhini. Hakika Allaah Hapendi mafisadi.

 

 

 

 

قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ الْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا ۚ وَلَا يُسْأَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٧٨﴾

78. (Qaaruwn) akasema: Hakika nimepewa haya kwa sababu ya ilimu yangu. Je, hajui kwamba Allaah Ameangamiza kabla yake karne ambazo zilikuwa ni zenye nguvu zaidi kuliko yeye na zenye mkusanyiko (wa mali) mwingi zaidi?  Na wala hawatoulizwa kuhusu dhambi zao wahalifu.

 

 

 

 

 

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾

79. Akawatokea watu wake katika pambo lake. Wale wanaotaka uhai wa dunia wakasema: Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kuu.

 

 

 

 

وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na wale waliopewa ilimu wakasema: Ole wenu! Thawabu za Allaah ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri.

 

 

 

 

فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنتَصِرِينَ ﴿٨١﴾

81. Basi Tukamdidimiza yeye na nyumba yake ardhini. Basi hakikuweko kikosi chochote cha kumnusuru dhidi ya Allaah, na wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru.

 

 

 

 

وَأَصْبَحَ الَّذِينَ تَمَنَّوْا مَكَانَهُ بِالْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ ۖ لَوْلَا أَن مَّنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na wakapambaukiwa wale waliotamani mahali pake jana, wakisema: Ee kumbe Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye kati ya Waja Wake na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Ingelikuwa Allaah Hakutufanyia fadhila, bila shaka Angelitudidimiza. Ee kumbe makafiri hawafaulu!

 

 

 

 

تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾

83. Hiyo ni nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi wala ufisadi. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.

 

 

 

 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾

84. Atakayeleta jema, basi atapata bora kuliko hilo. Na atakayeleta ovu, basi hawalipwi wale wanaotenda maovu isipokuwa yale waliyokuwa wanayatenda.

 

 

 

 

إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ مَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٨٥﴾

85. Hakika Yule Aliyekufaridhishia Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) bila shaka Atakurudisha mahali pa marejeo (Makkah). Sema: Rabb wangu Anamjua zaidi yule aliyekuja na hidaya na yule aliyemo katika upotofu bayana.

 

 

 

 

وَمَا كُنتَ تَرْجُو أَن يُلْقَىٰ إِلَيْكَ الْكِتَابُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na wala hukuwa unataraji kwamba utapewa Kitabu isipokuwa ni Rehma kutoka kwa Rabb wako. Basi usijekuwa msaidizi kwa makafiri.

 

 

 

 

وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ آيَاتِ اللَّـهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ ۖ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٨٧﴾

87. Na wala wasikuzuie kabisa kufuata Aayaat za Allaah baada ya kuteremshwa kwako. Na lingania kwa Rabb wako, na wala usiwe miongoni mwa washirikina.

 

 

 

وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۘ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na wala usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwingine. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Wajihi[8] Wake. Hukumu ni Yake Pekee na Kwake Pekee mtarejeshwa.[9]

 

[1] الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).

 

[2] Istighaathah (Kuomba Uokozi):

 

Rejea Al-Anfaal (8:9) kupata maana ya Istighaathah. Na kuhusu Isti’aanah, rejea Al-Faatihah (1:5).

 

[3] Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Anaomba Rizki Kwa Allaah:

 

Kama vile chakula kwani njaa ilikuwa imemshika sana. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[5] Wanaoiamini Qur-aan Katika Waliopewa Kitabu:

 

Ni watu wa Injiyl (Manaswara) na Tawraat (Mayahudi) ambao wameiamini Qur-aan na Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), hawakubadili wala hawakugeuza (Qur-aan). [Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[6] Haramisho La Kumuombea Maghfirah Kafiri:

 

Rejea At-Tawbah (9:113-114).

 

Aayah hii imeteremshwa kumhusu ammi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

عَنْ اِبْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ; جَاءَهُ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَعِنْدَهُ عَبْدُ اَللَّهِ بْنُ أَبِي أُمِّيَّةَ وَأَبُو جَهْلٍ فَقَالَ لَهُ: ((يَا عَمِّ قُلْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اَللَّهِ)) فَقَالاَ لَهُ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ؟ فَأَعَادَ عَلَيْهِ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَعَادَا، فَكَانَ آخَرَ مَا قَالَ: هُوَ عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ فَقَالَ اَلنَّبِيُّ  (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ)). فَأَنْزَلَ اَللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ)) وَأَنْزَلَ اَللَّهُ فِي أَبِي طَالِبٍ: ((إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ))

Amesimulia Ibn Al-Musayyib (رضي الله عنه)  kutoka kwa baba yake: Mauti yalipomkaribia Abuu Twaalib, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwendea akamkuta ‘Abdullaah bin Abiy Umayyah na Abuu Jahl wakiwa pamoja naye. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee ‘ammi yangu! Sema Laa ilaaha illa-Allaah, nitakuombea shafaa’ah kwa neno hili kwa Allaah.” Wawili hao wakamwambia: Utaacha dini ya (baba yako) ‘Abdul-Muttwalib? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akakariri (ombi lake) na wawili hao wakakariri nao vile vile. Ikawa neno la mwisho alilosema ni kubakia katika dini ya ‘Abdul-Muttwalib. Akafariki akiwa amekataa kusema Laa ilaaha illa-Allaah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nitaendelea kukuombea maghfirah madamu sijakatazwa kufanya hivyo.” Hapo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:

 

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾

Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa motoni.” [At-Tawbah: (9:113)]

 

Kisha Akateremsha kuhusu Abuu Twaalib:

 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

“Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye, lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.” [Al-Qaswasw (28:56) – Hadiyth katika Al-Bukhaariy]

 

[7] Qaaruwn:

 

Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.

 

Qaaruwn alikuwa miongoni mwa watu wa Muwsaa, yaani kutoka Bani Israaiyl. Salaf wametaja uhusiano wake na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام)  kuwa ni ammi yake au bin ammi yake. Na kauli iliyo na nguvu kabisa ni kuwa yeye ni bin ammi yake. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Qaaruwn alijaaliwa mali nyingi mno. Akatakabari kwa hazina hiyo na kukufuru Neema ya Allaah badala ya kushukuru, na akawa na batra na akajigamba kuwa mali hiyo amepewa kutokana ilimu yake (Aayah namba 78). Hayo yakampelekea kuwa muasi na dhalimu.  Na kwa ajili hiyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtaja pamoja na madhalimu na makafiri wengineo ambao ni Firawni na Haamaan (waziri wa Firawni) katika Suwrah Ghaafir (40:24), na Al-‘Ankabuwt (29:39). Na katika Suwrah hii ndio kisa chake kimeelezewa, na mwisho wake akadidimizwa katika ardhi.

 

Mali yake ikamshughulisha mno na akapinduka mipaka katika kibri chake. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya kuwa mtu kama huyo anayeshughulishwa na mali akaacha Swalaah, atafufuliwa pamoja na watu wa aina hii:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بن العاص عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ ذَكَرَ الصَّلاةَ يَوْمًا فَقَالَ:  ((مَنْ حَافَظَ عَلَيْهَا كَانَتْ لَهُ نُورًا وَبُرْهَانًا وَنَجَاةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ لَمْ يُحَافِظْ عَلَيْهَا، لَمْ يَكُنْ لَهُ نُورٌ وَلا بُرْهَانٌ وَلا نَجَاةٌ وَكَانَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ قَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَأُبَيِّ بْنِ خَلَفٍ)) أخرجه الإمام أحمد في مسنده

Amesimulia 'Abdullaah bin 'Amr ibn Al-'Aaasw (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitaja kuhusu Swalaah akasema: “Atakayeihifadhi atakuwa na nuru na uongofu, na kufuzu siku ya Qiyaamah. Na asiyeihifadhi, hatokuwa na nuru wala uongofu wala kufuzu, na siku ya Qiyaamah atakuwa pamoja na Qaaruwn, Firawni, Haamaan na Ubayy bin Khalaf.” [Musnad Ahmad ikiwa na Isnaad Swahiyh]

 

Katika kuifasiri Hadiyth hii, Ibn Al-Qayyim Al-Jawziy  (رحمه الله) amesema: “Mwenye kuacha Swalaah huwa ameshughulika na mojawapo kati ya yafuatayo: Ima atakuwa imemshughulisha mali yake, au ufalme wake, au cheo chake, au biashara zake. Yule aliyeshughulika na mali yake, atafufuliwa pamoja na Qaaruwn, na aliyeshughulika na ufalme wake, huyo atakuwa pamoja na Firawni, na aliyeshughulika na cheo chake atakuwa pamoja na Haamaan, na yule aliyeshughulika na biashara zake (akaacha kuswali), huyo atakuwa pamoja na Ubayy bin Khalaf.”

 

[8] Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibtiisha Sifa Za Allaah.

 

Rejea  Huwd (11:37), Al-Fat-h (48:10).

 

Na katika Sunnah,  Sifa hii ya Wajihi pia imethibitishwa kwenye du’aa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kwenye Hadiyth. Miongoni mwa Hadiyth hizo ni:

 

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى، قَالَ قَامَ فِينَا رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ فَقَالَ ‏ "‏ إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنَامُ وَلاَ يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ يَخْفِضُ الْقِسْطَ وَيَرْفَعُهُ يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْلِ حِجَابُهُ النُّورُ لَوْ كَشَفَهُ لأَحْرَقَتْ سُبُحَاتُ وَجْهِهِ مَا انْتَهَى إِلَيْهِ بَصَرُهُ مِنْ خَلْقِهِ ‏"‏ ‏.‏

Amesimulia Abuu Muwsaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama kati yetu na akasema mambo matano:  Akasema: “Allaah Halali, na wala haiwezekani Kwake kulala. Anateremsha Mizani na kuziinua. Amali inayotendwa usiku inapandishwa Kwake kabla ya amali inayotendwa mchana, na amali ya mchana (inapandishwa) kabla ya usiku.  Pazia Lake ni Nuru, na lau kama Angeliliondoa, basi Utukufu wa Wajihi Wake ungeunguza vitu vyote Alivyoviumba ambavyo Jicho Lake Limevizunguka vyote.” [Muslim, Ibn Maajah] 

 

[9] Viumbe Vyote Vitakufa Atabakia Allaah (عزّ وجلّ) Pekee:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anafahamisha kwamba watu wote wa ardhini watakufa na vivyo hivyo watu wa mbinguni isipokuwa kwa Amtakaye Allaah, na hakuna atakayesalia isipokuwa Wajihi Wake (سبحانه وتعالى) kwani Yeye ni Aliye Hai daima wala Hafi kamwe! [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Rejea pia Ghaafir (40:16) kupata faida ziyada.

 

 

Share