072 - Al-Jinn

 

  الْجِنّ

 

072-Al-Jinn

 

072-Al-Jinn: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾

1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.[1]

 

 

 

 

يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

2. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb wetu na yeyote.

 

 

 

وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾

3. Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.

 

 

 

 

وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا﴿٤﴾

4. Na kwamba safihi miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Allaah uongo uliopinduka mipaka.

 

 

 

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا﴿٥﴾

5. Na hakika sisi tulidhania kuwa wanaadam na majini hawatosema uongo juu ya Allaah.

 

 

 

 

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾

6. Na kwamba wanaume miongoni mwa wanaadam walikuwa wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.

 

 

 

 

وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا﴿٧﴾

7. Na kwamba wao walidhania kama mlivyodhani nyinyi kwamba Allaah Hatomfufua yeyote (au Hatomtuma Rasuli).

 

 

 

 

وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا﴿٨﴾

8. Na kwamba sisi tulitafuta kuzifikia mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinzi wakali na vimondo.

 

 

 

 

وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا﴿٩﴾

9. Na kwamba sisi tulikuwa tukikaa huko vikao kwa ajili ya kusikiliza, basi atakayetega sikio kusikiliza sasa atakuta kimondo kinamvizia.

 

 

 

 

وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا﴿١٠﴾

10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa ardhini, au Rabb wao Anawatakia uongofu.

 

 

 

 

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا﴿١١﴾

11. Na kwamba miongoni mwetu wako walio wema, na miongoni mwetu wako walio kinyume chake, nasi tumekuwa makundi ya njia mbali mbali.

 

 

 

 

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا﴿١٢﴾

12. Na sisi tulikuwa na yakini kwamba hatutoweza kumshinda Allaah ardhini, na wala hatutoweza kumkwepa kutoroka.

 

 

 

 

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ ۖ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا﴿١٣﴾

13. Na kwamba sisi tuliposikia mwongozo (hii Qur-aan) tuliuamini. Basi atakayemuamini Rabb wake, hatoogopa kupunjwa mazuri yake wala kuzidishiwa adhabu ya madhambi.

 

 

 

 

وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا﴿١٤﴾

14. Na kwamba miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu ni wakengeukaji haki. Hivyo atakayesilimu, hao ndio waliofuata kidhati uongofu.

 

 

 

 

وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا﴿١٥﴾

15. Ama wakengeukaji haki, hao watakuwa kuni za Jahannam.

 

 

 

 

وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا﴿١٦﴾

16. (Allaah Anasema):  Na kwamba lau wangelinyooka kwenye njia, bila shaka Tungeliwanywesha maji kwa wingi.

 

 

 

 

لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا﴿١٧﴾

17. Ili Tuwatie katika jaribio kwayo. Na anayepuuza Ukumbusho wa Rabb wake, Atamsukuma kwenye adhabu ngumu ya kumlemea asiiweze.

 

 

 

 

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

18. Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah tu, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.[2]

 

 

 

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا﴿١٩﴾

19. Na kwamba Mja wa Allaah (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama kumwomba (Rabb wake), walikaribia kwa mlundikano wao kumzonga.

 

 

 

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾

20. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.

 

 

 

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾

21. Sema: Hakika mimi sikumilikieni dhara wala uongofu.

 

 

 

 

قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا﴿٢٢﴾

22. Sema: Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia ila Kwake tu.

 

 

 

 

إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ ۚ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا﴿٢٣﴾

23. Isipokuwa nibalighishe (haki) kutoka kwa Allaah na Ujumbe Wake. Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Rasuli Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam, watadumu humo abadi.

 

 

 

 

حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا﴿٢٤﴾

24. Mpaka watakapoona yale wanayoahidiwa sasa, basi watajua ni nani msaidizi dhaifu, na mchache zaidi kwa idadi.

 

 

 

 

قُلْ إِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُ رَبِّي أَمَدًا﴿٢٥﴾

25. Sema: Mimi sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Rabb wangu Atayaweka muda mrefu.

 

 

 

 

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا﴿٢٦﴾

26.  Mjuzi wa ghaibu, na wala Hamdhihirishii yeyote Ghaibu Yake.[3]

 

 

 

 

إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا﴿٢٧﴾

27. Isipokuwa Rasuli ambaye Yeye Amemridhia. Basi hakika Yeye Anamwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

 

 

 

 

لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا﴿٢٨﴾

28. Ili Ajue kwamba wamekwishabalighisha   Ujumbe wa Rabb wao, na Ameyazunguka (kwa Ujuzi Wake) yale waliyo nayo, na Ametia hesabuni barabara idadi ya kila kitu.

 

 

 

 

[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

072-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Jinn: قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا

 

Na kisa hiki cha majini kusikiliza Qur-aan, ikawashangaza, na kuilingania kwa majini wenzao, kimetajwa pia katika Suwrah Al-Ahqaaf (46:29-32).

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ انْطَلَقَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فِي طَائِفَةٍ مِنْ أَصْحَابِهِ عَامِدِينَ إِلَى سُوقِ عُكَاظٍ، وَقَدْ حِيلَ بَيْنَ الشَّيَاطِينِ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، وَأُرْسِلَتْ عَلَيْهِمُ الشُّهُبُ، فَرَجَعَتِ الشَّيَاطِينُ إِلَى قَوْمِهِمْ‏.‏ فَقَالُوا مَا لَكُمْ فَقَالُوا حِيلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، وَأُرْسِلَتْ عَلَيْنَا الشُّهُبُ‏.‏ قَالُوا مَا حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ إِلاَّ شَىْءٌ حَدَثَ، فَاضْرِبُوا مَشَارِقَ الأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا، فَانْظُرُوا مَا هَذَا الَّذِي حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ فَانْصَرَفَ أُولَئِكَ الَّذِينَ تَوَجَّهُوا نَحْوَ تِهَامَةَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ بِنَخْلَةَ، عَامِدِينَ إِلَى سُوقِ عُكَاظٍ وَهْوَ يُصَلِّي بِأَصْحَابِهِ صَلاَةَ الْفَجْرِ، فَلَمَّا سَمِعُوا الْقُرْآنَ اسْتَمَعُوا لَهُ فَقَالُوا هَذَا وَاللَّهِ الَّذِي حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ‏.‏ فَهُنَالِكَ حِينَ رَجَعُوا إِلَى قَوْمِهِمْ وَقَالُوا يَا قَوْمَنَا ‏ ‏إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا‏}‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{‏قُلْ أُوحِيَ إِلَىَّ‏}‏ وَإِنَّمَا أُوحِيَ إِلَيْهِ قَوْلُ الْجِنِّ‏.‏

Amesimulia Ib ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka akikusudia kwenda soko la ‘Ukaadhw akifuatana na baadhi ya Swahaba. Wakati huo huo, kizuizi kiliwekwa kati ya mashaytwaan na khabari za mbinguni. Vimondo vya moto vikaanza kurushwa kwao. Mashaytwaan yalikwenda kwa watu wao, kuwauliza: “Mna tatizo gani?” Wakasema: “Kizuizi kimewekwa kati yetu na khabari za mbinguni. Na tumevurumishwa vimondo vya moto.” Wakasema: “Kitu kilichoweka kizuizi kati yenu na khabari za mbinguni kitakuwa kimetokea hivi karibuni. Nendeni upande wa Mashariki na Magharibi ili muone kizuizi kilichowekwa kati yenu na taarifa za mbinguni.” Wale walioelekea Tuhaamah walipita kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa katika eneo linaitwa Nakhlah, wakielekea soko la ‘Ukaadhw. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiwaswalisha Swahaba zake Swalaah ya Alfajiri.  (Majini) waliposikia Qur-aan inasomwa, wakasikiliza kwa makini wakasema: “Hii wa-Allaahi ndio iliyokuwekeeni kizuizi baina yenu na baina ya khabari za mbingu.” Pindi waliporudi kwa watu wao wakasema: “Enyi kaumu yetu!

 

إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾ يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

“Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote.” [Al-Jinn (72:2)]

 

Allaah Akamteremshia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. [Al-Jinn (72:1)]

 

[2] Kumshirikisha Allaah:  

 

Kumshirikisha Allaah (عزّ وجلّ) ni madhambi pekee ambayo Allaah Hamghufurii mtu isipokuwa akitubia kabla ya  kufariki au kabla ya jua kuchomoza upande wa Magharibi. Bonyeza kiungo kifuatacho kupata maelezo yake:

 

048-Aayah Na Mafunzo: Allaah Hamghufurii Mja Atakayefariki Bila Ya Kutubia Katika Kumshirikisha

 

Bonyeza pia viungo vifuatavyo vyenye faida tele kuhusu shirki ya kuwaomba wasiokuwa Allaah:

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!- إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

 

048-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Haki Ya Allaah Ni Kumwabudu Bila Kumshirikisha Na Kitu

 

23-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Haijuzu Kutawassal Kwa Jaha Ya Nabiy

 

24-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Waja Wema Waliofariki

 

25-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa 'Ahlul-Badr' Watu wa Badr

 

33-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Majini Na Mazimwi

 

[3] Hakuna Ajuaye Ghaibu Isipokuwa Allaah:

 

Rejea An-Naml (27:65).

 

 

 

 

 

Share