083 - Al-Mutwaffifiyn

  الْمُطَفِّفِين

 

083-Al-Mutwaffifiyn

 

 

 083-Al-Mutwaffifiyn: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾

1. Ole kwa wanaopunja.[1]

 

 

 

الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾

2. Ambao wanapopokea kipimo kwa watu wanataka wapimiwe kamilifu.

 

 

 

وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾

3. Na wanapowapimia (watu) kwa kipimo au wanawapimia kwa mizani wanapunja.

 

 

 

أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾

4. Je, hawadhanii kwamba wao watafufuliwa?

 

 

لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾

5. Kwenye Siku iliyo kuu kabisa.

 

 

يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾

6. Siku watakayosimama watu kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

 

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾

7. Laa hasha! Hakika kitabu cha watendaji dhambi bila shaka kimo katika Sijjuwn.[2]

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾

8. Na lipi litakalokujulisha nini Sijjuwn?

 

 

 

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾

9.  Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara (matendo). 

 

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾

10. Ole Siku hiyo kwa wakadhibishaji.

 

 

 

الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿١١﴾

11. Ambao wanaikadhibisha Siku ya malipo.

 

 

 

 

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾

12. Na haikadhibishi isipokuwa kila mwenye kutaadi, mtendaji dhambi.

 

 

 

 

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾

13. Anaposomewa Aayaat Zetu, husema: Hekaya za watu wa kale.

 

 

 

 

كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

14. Laa hasha! Bali yamefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma.[3]

 

 

 

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ ﴿١٥﴾

15. Laa hasha! Hakika wao Siku hiyo bila shaka watawekewa kizuizi wasimuone Rabb wao.[4]

 

 

 

ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ﴿١٦﴾

16. Kisha hakika wao bila shaka wataingizwa na waungue katika moto uwakao vikali mno.

 

 

 

ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿١٧﴾

17. Kisha itasemwa: Haya ndio yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.

 

 

 

 

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾

18. Laa hasha! Hakika kitabu cha Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka kiko katika ‘Illiyyuwn.[5]

 

 

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ ﴿١٩﴾

19. Na lipi litakalokujulisha nini hiyo ‘Illiyyuwn?

 

 

 

 

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٢٠﴾

20. Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara (amali).

 

 

 

 

يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢١﴾

21. Watakishuhudia waliokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

 

 

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿٢٢﴾

22. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka watakuwa kwenye neema (taanasa, furaha n.k).

 

 

 

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Kwenye makochi ya fakhari wakitazama.

 

 

 

 

تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾

24. Utatambua nyuso zao kwa nuru ya neema (taanasa, furaha).[6]

 

 

 

 

يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ ﴿٢٥﴾

25. Watanyweshwa kinywaji safi na bora kabisa cha mvinyo kilichozibwa.

 

 

 

 

خِتَامُهُ مِسْكٌۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾

26. Mwisho wake ni miski. Na katika hayo basi washindane wenye kushindana.

 

 

 

وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ ﴿٢٧﴾

27. Na mchanganyiko wake ni kutokana na Tasniym.

 

 

 

 

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢٨﴾

28. Ni chemchemu watakayokunywa humo watakaokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ ﴿٢٩﴾

29. Hakika wale waliofanya uhalifu walikuwa (duniani) wakiwacheka wale walioamini.

 

 

 

وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na wanapowapitia wanakonyezana.

 

 

 

 

وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ ﴿٣١﴾

31. Na wanaporudi kwa ahli zao, hurudi wenye kufurahika kwa dhihaka.

 

 

 

 

 

وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ ﴿٣٢﴾

32. Na wanapowaona, husema: Hakika hawa bila shaka ndio waliopotea.

 

 

 

 

وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾

33. Na wao hawakutumwa kuwa ni walinzi juu yao.

 

 

 

 

 

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴿٣٤﴾

34. Basi leo wale walioamini watawacheka makafiri.

 

 

 

 

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Kwenye makochi ya fakhari wakitazama.

 

 

 

 

هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Je, basi makafiri wamelipwa yale waliyokuwa wakiyafanya? 

 

 

 

 

[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

083-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Mutwaffifiyn Aayah 1-6: وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ

 

Upunjaji mizani katika uuzaji wa bidhaa ni uasi na dhulma kubwa ambayo walikuwa wakitenda pia watu wa Nabiy Shu’ayb   (عليه السّلام)   akawalingania watu wake waache dhulma hiyo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ﴿٨٤﴾ وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ﴿٨٥﴾

Na kwa Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Na wala msipunguze kipimo na mizani. Hakika mimi nakuoneni mko katika kheri (na neema), na hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku yenye kuzingira.  Na enyi kaumu yangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu, na wala msipunje watu vitu vyao, na wala msifanye uovu katika ardhi mkawa mafisadi. [Huwd (11:84-85)]

 

[2] Moto Wa Jahannam Uko Sijjuwn Na Jannah Iko ‘Illiyyuwn:

 

Amesema Al-A’mash kutoka kwa Shamar bin ‘Atwiyyah kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf amesema: Ibn ‘Abbaas alimuuliza Ka’ab (رضي الله عنهما)  nami nilikuwepo kuhusu Sijjuwn, akasema: “Hiyo ni ardhi ya saba, na humo kuna roho za makafiri.” Na  akamuuliza kuhusu 'Illiyyuwn, naye akasema: “Hiyo ni mbingu ya saba na humo kuna roho za Waumini.” Na wengineo wamesema pia kuwa ni mbingu ya saba.  Kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى): 

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾

Laa hasha! Hakika kitabu cha Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka kiko katika ‘Illiyyuwn.

  

[‘Aliy bin Abiy Twalhah akipokea toka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Yaani ni Jannah (Pepo). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema: “Jannah iko juu ya 'Illiyyuwn na moto wa Jahannam uko katika Sijjuwn, na Sijjuwn ni chini kabisa ya ardhi. Kama isemavyo Hadiyth "Anapokufa mtu, Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema: Kirekodi kitabu cha mja Wangu katika Sijjuwn chini kabisa ya ardhi."

 

Ama Jannah iko juu, juu kabisa ya 'Illiyyuwn.

 

Na imethibiti kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "'Arsh ya Rabb (سبحانه وتعالى) Aliyetukuka Aliye juu, ni sakafu ya Jannah ya Al-Firdaws."

[Fataawa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb (4/2)]

 

[3] Dhambi Zinapozidi Hutia Kutu Katika Nyoyo Mpaka Zinapofuka Kwa Madhambi:

 

Binaadam anapotenda dhambi, anapaswa kukimbilia istighfaar (kuomba maghfirah) na kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى), kwani kuchelewa kufanya hivyo na akaendelea mtu kutenda madhambi, moyo wake huingia kutu na hatimae hupofuka kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أبي هُرَيرة، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ العبدَ إذا أخطأَ خطيئةً نُكِتت في قلبِهِ نُكْتةٌ سوداءُ، فإذا هوَ نزعَ واستَغفرَ وتابَ سُقِلَ قلبُهُ، وإن عادَ زيدَ فيها حتَّى تعلوَ قلبَهُ، وَهوَ الرَّانُ الَّذي ذَكَرَ اللَّه عز وجل ((كَلاَّ بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) رواه أحمد والترمذي وحسنه الألباني

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mja anapofanya dhambi, doa jeusi (kutu) huwekwa katika moyo wake.  Akiacha dhambi hiyo, na kuomba maghfirah na kutubu, moyo wake husafishwa ukawa msafi, lakini akirudia kufanya dhambi, doa (kutu) huzidi kuenea mpaka kufunika moyo wote na hiyo ndio 'Raan' (kutu) Aliyoisema Allaah (عزّ وجلّ):

 

كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

Laa hasha! Bali yamefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma [Al-Mutwaffifiyn (83:14)] [Ahmad, At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hasan]

 

[4] Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Kuamini Kwamba Waumini Watamuona Allaah Watakapokuwa Jannah:

 

Imaam Abiy ‘Abdillaah Ash-Shaafi’iy (رحمه الله) amesema: “Hii ni dalili kwamba Waumini watamuona Allaah (عزّ وجلّ) Siku hiyo.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Rejea Yuwnus (10:26) kwenye dalili nyenginezo bayana za Waumini kumuona Rabb wao.  Rejea pia Suwrah Al-Qiyaamah (75:22-23).

 

[5] Illiyyuwn Ni Mahala Katika Jannah

 

Rejea Aayah namba (7) ya Suwrah hii kwenye faida.  

 

[6] Nyuso Za Waumini Zitang’ara Kwa Furaha Siku Ya Qiyaamah:

 

Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye kubainisha hali za nyuso za Waumini na makafiri zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah.

 

 

 

 

Share