106 - Quraysh

 

  قُرَيْش

 

106-Quraysh

 

106-Quraysh: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ ﴿١﴾

1. (Tumewaangamiza watu wa tembo) ili Maquraysh wapate kuendelea na mazoea.[1]

 

 

إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ ﴿٢﴾

2. Mazoea yao ya safari (za kibiashara) za majira ya baridi na majira ya joto.

 

 

 

 

فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَـٰذَا الْبَيْتِ ﴿٣﴾

3. Basi wamuabudu Rabb wa Nyumba hii (Ka’bah).

 

 

الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ ﴿٤﴾

4. Ambaye Anawalisha kuwaokoa na njaa, na Anawapa amani kutokana na khofu.

 

 

[1] Suwrah Hii Kuhusiana Na Ya Al-Fyl:

 

Wafasiri wengi wamesema kwamba Suwrah hii inaunganishwa na Suwrah iliyotangulia (ya Al-Fiyl). Na maana yake ni: Tulifanya yale Tuliyowafanyia jeshi la tembo kwa ajili ya maquraysh ili kuwahifadhi salama, kulinda maslahi yao na usalama wa safari zao za kawaida kwenda Yemen katika majira ya baridi na Sham wakati wa kiangazi, kwa madhumuni ya biashara na chumo. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Rejea Utangulizi Wa Suwrah kupata faida.

 

 

 

Share