107 - Al-Maa’uwn

 

  الْمَاعُون

 

107-Al-Maa’uwn

 

 

107-Al-Maa’uwn: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾

1. Je, umemuona yule anayekadhibisha malipo?

 

 

فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾

2. Basi huyo ndiye yule anayemnyanyasa yatima.  

 

 

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾

3. Na wala hahamasishi kulisha maskini.

 

 

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾

4. Basi ole kwa wanaoswali.

 

 

الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾

5. Ambao wanapuuza Swalaah zao.

 

 

الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿٦﴾

6. Ambao wanajionyesha (riyaa).[1]

 

 

وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ ﴿٧﴾

7. Na wanazuia (pia) misaada ya matumizi madogodogo ya kawaida ya kila siku.

 

 

[1] Riyaa (Kujionyesha Kwa Watu):

 

Riyaa ni kujionyesha kwa watu matendo mema badala ya kumsafishia niyah Allaah. Hii ni aina ya shirki ndogo ambayo inabatilisha amali.

 

Rejea Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki.

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya katika Hadiyth kadhaa kuhusu riyaa, miongoni mwazo ni:

 

عَنْ جُنْدَبِ بْنِ عَبْدُ الله بْنِ سُفْيانَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ سَمَّعَ سَمَّعَ اللَّهُ بِهِ وَمَنْ رَاءَى رَاءَى اللَّهُ بِهِ)) متفق عليه

Amesimulia Jundab bin ‘Abdillaah bin Sufyaan (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuzungumza (au kusoma) ili watu wamsifu, Allaah Atamfedhehesha Siku ya Qiyaamah, na mwenye kuwafanyia watu riyaa (kwa amali njema ili aonekane ni mtukufu), Allaah Atazidhihirisha siri zake (Siku ya Qiyaamah).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 Na katika Qur-aan imetajwa riyaa za watu katika ibaada mbali mbali: Rejea Al-Baqarah (2:264), An-Nisaa (4:38), (4:142), na Al-Anfaal (8:47).

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuacha kutufundisha jinsi ya kujikinga na riyaa, akatufundisha duaa ifuatayo:

اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ أَنْ أُشْـرِكَ بِكَ وَأَنا أَعْـلَمْ، وَأَسْتَـغْفِرُكَ لِما لا أَعْـلَم

Ee Allaah! Hakika mimi Najikinga Kwako kutokana na kukushirikisha hali ya kuwa najua, na ninakuomba maghfira kwa nisiyoyajua.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo kupata makala kuhusu shirki ya riyaa:

 

Riyaa (Shirki Iliyofichikana)

 

02-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Ni Aina mbili Na Tofauti Zake

 

03-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Ndogo - Riyaa (Kujionyesha)

 

04-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Inabatilisha ‘Amali

 

05-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Hatima Ya Mwenye Riyaa (Kujionyesha)

 

 

 

 

Share