Ukimbizi Na Kubadilisha Jina La Baba

SWALI:

Assalam alaykum

Napenda kuuliza suali. Mimi naishi London maisha yetu sisi huku huwa tunakwenda magration na kuomba ukimbizi kwa kubadilisha uraia(mfano mkenya unasema wewe unatoka somali) sasa wakati tunapoulizwa majina yetu huwa tunabadilisha majina kama mtu unaitwa Khadija Ali basi unabadilisha jina la baba unasema unaitwa Khadija Ahmed sasa je inakubalika kiislam na kama haikubaliki tufanye nini? kwa upande wangu binafsi nimebadili jina la baba kwa nchi hii naitwa jina jingene lakini nyumbani najiita jina jengine hili nalitumia kwa hapa tu sasa je Mwezi Mungu atatuweka katika watu wa fungu gani? Naomba majibu na hivi kubadilisha uraia ni sahihi? lakini Dini sijabadilisha nimesema ni Muislam.

 


 

 

JIBU:  

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Kulingana na mafunzo ya Kiislamu kudanganya ni haramu, Kubadilisha uraia hakuna ubaya lakini kusiwe kinyume cha Sheria ya Kiislamu kwa mfano; kwa njia ya udanganyifu na kadhalika.

Ile nchi uliotoka ikiwa unafanya hijra (kuhama) kwa sababu ya kudhulumiwa kwa ibada au haki nyiginezo uhame kwenda nchi ambayo utapata uhuru wa kuendesha ibada zako bila pingamizi zozote, kupata hali ya kimaisha bora, na kadhalika. Lakini kuhama huku kusiwe kwa gharama ya dini yako.  

Asli katika Uislamu, Hijra ni kuhama kutoka nchi ya kikafiri kwenda katika nchi ya Kiislamu au ya Waislamu. Mtu kubadalisha jina la babake haifai, Allaah سبحانه وتعالى  Amesema:

}}ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ{{ 

 {{Waiteni kwa (majina ya) baba zao, maana huo ndio uadilifu mbele ya Mwenyezi  Mungu}}

  Ahzaab 33:5

 Wa Allaahu A'alam

 

Share