Kutumia Credit Card

SWALI:

Je nauliza ni hukmu ya Credit Card kama huta lipa riba yaani ukilipa deni kabla muda ulopewa haujamalizikaJIBU:

 

AlhamduliLLaah,  Waswalaatu Was-salaam 'alaa Rasuuli-Llaah  صلى الله عليه وآله وسلم Amma ba'ad,

Hukumu ya Credit Card ni haraam hata kama mtumiaji atahakikisha kuwa atalipa mkopo aliopewa ndani ya kadi hiyo benki kabla ya muda aliopewa haujamalizika. Hii ni kwa sababu mtumiaji anaingia katika mkataba kuwa ikiwa atachelewa kulipa deni alipe kwa faida (riba).  Na Muislamu hatakiwi kuingia katika mkataba wa jambo la haraam.

 

Mwanachuoni Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Allaah Amrehemu) aliulizwa kuhusu mkataba kama huu akasema: "Makubaliano  kama haya ni haraam kwa sababu mtu anayeingia katika makubaliano haya anajishurutisha kulipa riba kama hakuweza kulipa kwa wakati wake.  Kujishurutisha hivi haifai hata kama anafikiri kwamba atalipa deni kabla ya wakati wake kufika kwa sababu hali inaweza kubadilika na asiweze kulipa. Haya ni mambo ya mbele ambayo hakuna anayejua hali yake itakuwa vipi siku za mbele.  Kwa hiyo mkataba kama huu ni haraam". 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share