Kumchora Mtoto Mchanga Usoni Kwa Ajili Ya Kinga

 

Kumchora Mtoto Mchanga Usoni Kwa Ajili Ya Kinga

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Asalaam alykum  naomba kuulza nn hukmu ya kumchora mtoto usoni akiwa mchanga? Utamadun huo umeenea sana kwa sisi maibadhi hasa Oman.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Jambo hilo linalofanywa na baadhi ya jamii  ya watu kuwachora watoto wachanga usoni kwa kuitakidi kuwa ni kinga ya husda au jicho baya, ni jambo zaidi la kimila na itikadi za tamaduni fulani na si la Kiislamu.

 

Jambo hilo halifai, bali kufanya hivyo ni miongoni mwa shirki kubwa mno zinazomuangamiza mtu.

 

Kwa faida zaidi soma maelezo bayana katika kifungo kifutaacho:

 

14-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kuvaa Kitu Kwa Ajili Ya Kinga

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha jambo ila ameshalifundisha. Alikuwa akiwakinga wajukuu wake Al-Hasan na Al-Husayn kwa kuwasomea:

 

أُعيـذُكُمـا بِكَلِـماتِ اللهِ التّـامَّة، مِنْ كُلِّ شَيْـطانٍ وَهـامَّة، وَمِنْ كُـلِّ عَـيْنٍ لامَّـة

U’iydhukumaa bikalimaatiLLaahit-ttaammati min kulli shaytwaanin wa haammah, wa min kulli ’aynin laammah.
Nawakinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia Awakinge kutokana na kila shaytwaan na uvamizi na kila jicho lenye kudhuru.  [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ’anhumaa) Al-Bukhaariy (4/119) [3371].

 

Kwa hiyo ni vyema kushikamana na mafunzo sahihi ya Dini hii tukufu badala ya kufuata mila na tamaduni potofu na kujiingiza katika kupata ghadhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share