Al-Lajnah Ad-Daaimah: Maulidi: Hukmu Ya Kusherehekea Maulidi Ya Nabiy ﷺ
Hukmu Ya Kusherehekea Maulidi Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Katika Mwezi Wa Rabiy’ul-Awwal Kwa Ajili Ya Kumuadhimisha
Al-Lajnah Ad-Daa'imah
SWALI:
Nini hukmu ya kusherehekea mawlid ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika mwezi wa Rabiy’ul Awwal kwa ajili ya kumuadhimisha?
JIBU:
Kumuadhimisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumheshimu ni kwa kuamini kila alilokuja nalo kutoka kwa Allaah, na kufuata Shariy’ah Yake, ki-‘Aqiydah, na kwa kauli na kwa matendo na tabia, na kuacha bid’ah katika Dini.
Na katika mambo ya bid’ah ni kusherehekea Mawlid Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Wa biLLaahit-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fatwa (3257) – Al-Lajnah Ad-Daaimah]