Al-Lajnah Ad-Daaimah: Haijuzu Kwa Muislamu Kusherehekea ‘Iyd Zisizokuwa Za Kiislamu Wala Kushiriki Lolote

 

Haijuzu Kwa Muislamu Kusherehekea ‘Iyd Zisizokuwa Za Kiislamu

Wala Kushiriki Lolote

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Muislamu anayemwamini Allaah kuwa ni Rabb, na Uislamu kuwa ni Dini,  na kumwamini Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba ni Nabiy na Rasuli – haijuzu kwake kusherehekea ‘Iyd ambazo hazina asili katika Dini ya Kiislamu.

 

Wala haijuzu pia kuhudhuria au kushiriki humo wala kusaidia kwa lolote au chochote kwa sababu hivyo ni dhambi na ni kuvuka mipaka ya Allaah na Allaah (Ta’aalaa) Anasema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah : 2]

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (3825)]

 

 

 

Share