Al-Lajnah Ad-Daaimah: Vitabu Muhimu Kwa Mwanafunzi Wa Dini

 

Vitabu Muhimu Kwa Mwanafunzi Wa Dini

 

 

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni vitabu vipi muhimu kwa mwenye kutafuta elimu?

 

 

JIBU:

 

Usome Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ambacho kina uongofu, nuru na Sunnah ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni lazima usome vitabu vya Tafsiyr (ufafanuzi wa maana za Qur-aan) na vile (vitabu) vya sayansi ya Hadiyth kwa msaada wa Wanachuoni wabobezi.

 

Ni muhimu kufanyia kazi kwa yale unayojifunza. Yeyote anayefanyia kazi yale anayojifunza ataruzukiwa ‘ilm ya vitu ambavyo wao hawavifahamu.

 

Vitabu vifuatavyo vinahimizwa sana:

 

Vitabu Viwili Swahiyh vya Hadiyth (yaani Al-Bukhaariy na Muslim)

Buluughul-Maraam

‘Umdatul-Hadiyth cha ‘Abdul-Ghaniy bin ‘Abdil-Waahid Al-Maqdisy

Muntaqa Al-Akhbaar na Zaad Al-Ma’ad cha Ibn Al-Qayyim, na

Al-‘Aqiydah Al-Wasitwiyyah cha Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahum Allaahu), kwa kuongezea na:

Kitaab At-Tawhiyd

Kashf Al-Shubuhaat

na Fat-hul-Majiyd.

 

Allaah Atujaalie mafanikio.

 

Swalaah na Salaam za Allaah ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, ukoo wake na Maswahaba zake!

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah, Mjaladi wa 12, Jihaad na Hisbah, ’Ilm, Vitabu bora, Fatwa Namba 3534]

 

 

`Abdul-`Aziz bin `Abdillaah bin Baaz – Mwenyekiti

`Abdullaah bin Qa`uwd – Mjumbe

`Abdullaah bin Ghudayyaan – Mjumbe

 

Share