Imaam Ibn Baaz: Maulidi: Hukmu Ya Kuchinja Kwa Ajili Ya Maulidi

 

Hukmu Ya Kuchinja Kwa Ajili Ya  Maulidi

 

Imaam Bin Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kuchinja ambayo itakuwa ni siku ya mawlid?

 

 

JIBU:

 

Ikiwa kuchinja kwake ni kwa ajili ya Mawlid yake basi hiyo ni shirki kubwa.

 

Ama ikiwa kuchinjwa kwake ni kwa ajili ya kula tu, basi hakuna neno. Lakini inapasa kisiliwe (chakula hicho cha Mawlid), na asihudhurie Muislamu (kwenye sherehe za Mawlid na kwenye chakula cha Mawlid) kwa ajili ya kupinga kwa kauli na vitendo.

 

Isipokuwa tu kama atahudhuria kwa ajili tu ya kuwapa nasaha (ya kuacha bid'ah hiyo) bila kushiriki katika hilo la kula chakula (cha Mawlid).

 

 

[Imaam Bin Baaz, Majmuw' Al-Fataawaa (9/74)]

 

 

 

Share