Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukmu Ya Kuua Panya

Hukmu Ya Kuua Panya

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Unapotaka kuua panya - na kumuua ni jambo lenye kupendeza – basi umuue kwa njia nzuri.

 

Muue kwa njia ambayo itaitoa roho yake mara moja na si kumtesa.

 

Na yenye kumtesa, ni yale wanayoyafanya baadhi ya watu, ambapo wanaweka aina ya gundi ambayo inamnasa (na kumzuia kutoka) na kumfanya afe kwa njaa na kiu; na (kufanya hivyo) hakujuzu.

 

Utakapoiweka hiyo gundi, basi huna budi kurudi kuitazama na kuichunga (kila mara) mpaka utakapokuta kuna kitu (panya) kimenaswa ukiue (usiache ateseke).

 

Ama kuacha hiyo gundi kwa siku mbili au tatu na akaingia panya (mtegoni) na akafa kwa njaa au kiu, basi hukhofiwa juu yako kuingia motoni kwa sababu hiyo.

 

Kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

“Aliingia motoni mwanamke kwa sababu ya paka aliyemfungia ndani hadi akafa; hakumlisha wala hakumuacha aende kutafuta chakula kwa kula vijidudu vya ardhini.”

 

 

[Sharh Riyaadhw Asw-Swaalihiyn, 4/596]

 

Share