23-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

23 Je, Inajuzu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?

 

Hapana! Haijuzu kuweka nadhiri isipokuwa kwa sababu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ   

 “Rabb wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nitakabalie. [Aal-‘Imraan: 35]

 

((مَنْ نَذَرَ أَنْ يُطِيعَ اللَّهَ فَلْيُطِعْهُ ، وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَهُ فَلَا يَعْصِهِ))رواه البخاري

((Anayeweka nadhiri kumtii Allaah basi amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah basi asimuasi)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Share