39-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

39-Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?

 

Tukitaka kuombewa shafaa’ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inapasa tumuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  

 

قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ

Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah Pekee.  [Az-Zumar: 44]

 

((اللّهم شفّعه فيّ)) رواه الترمذي وقال حديث حسن.

((Ee Allaah! Ikubali shafaa’ah (maombezi) yake kwangu))

 

 

 

Share