40-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Vipi tumpende Allaah Na Rasuli Wake?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

40-Vipi tumpende Allaah Na Rasuli Wake?

 

Mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kutii na kufuata amri ya Allaah.

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ...

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah  [Aal-‘Imraan: 31]

 

((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ)) متفق عليه

((Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote waliobakia)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share