41-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy kwa kumpandisha cheo kama cha Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

41-Je, Inajuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy kwa kumpandisha cheo kama cha Allaah?

 

 Hapana! Haijuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka kumfikisha cheo cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee [Al-Kahf: 111]

 

((لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتْ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ فَقُولُوا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ)) متفق عليه

((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share