Nawaaqidhw Al-Islaam: Mambo (Kumi) Yanayomtoa Mtu Nje Ya Uislamu

 

Nawaaqidhw Al-Islaam

 

Mambo Yanayomtoa Mtu Nje Ya Uislamu

 

Muhammad  Bin 'Abdil-Wahhaab Sulaymaan At-Tamiymiy

 

Imetarjumiwa na

 

Alhidaaya.com

 

 

قال الإمام المجدد شيخ الإسلام محمد بن عبد الوهاب رحمه الله: اعلم أن نواقض الإسلام عشرة :

Imaam Al-Mujaddid Shaykhul-Islaam Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab (Rahimahu-Allaah) amesema:  Jua ya kwamba mambo yanayomtoa Muislamu nje ya Uislamu ni kumi.

 

 الأَوَّلُ: الشِّرْكُ فِي عِبَادَةِ اللهِ  

Kwanza: Kumshirikisha Allaah katika ‘ibaadah.

 

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.  Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu  [An-Nisaa: 48]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]

 

Miongoni mwayo ni kuchinja kwa kumkusudia asiyekuwa Allaah kama kuchinja kwa ajili ya majini na makaburi.

الثَّانِي: مَنْ جَعَلَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ اللهِ وَسَائِطَ يَدْعُوهُمْ وَيسْأَلُهُمْ الشَّفَاعَةَ، وَيَتَوَكَّلُ عَلَيْهِمْ كَفَرَ إِجْمَاعًا.

Pili: Mwenye kufanya baina yake na baina ya Allaah viunganishi akiviomba du’aa na kuviomba shafaa’ah (uombezi) na kutawakali kwavyo ni kufru kwa Ijmaa’aa (makubaliano ya ‘Ulamaa).

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa: 

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾

...na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamwongoi aliye muongo, kafiri mkubwa. [Az-Zumar: 3]

الثَّالِثُ: مَنْ لَمْ يُكَفِّرْ المُشْرِكِينَ أَوْ شَكَّ فِي كُفْرِهِمْ، أَوْ صَحَّحَ مَذْهَبَهُم،ْ كَفَرَ.

Tatu: Asiyewakufurisha washirikina au kutia shaka katika kufru zao au akausahihisha ukafiri wao, amekufuru. 

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٣٠﴾

Na Mayahudi wanasema: “‘Uzayr ni mwana wa Allaah”; na Manaswara wanasema: “Al-Masiyh (‘Iysaa) ni mwana wa Allaah.” Hiyo ni kauli yao kwa midomo yao. Wanaiga kauli ya wale waliokufuru kabla. Allaah Awaangamize! Basi namna gani wanavyoghilibiwa? [At-Tawbah: 30]

الرَّابِعُ: مَنْ اعْتَقَدَ أَنَّ غَيْرَ هَدْي النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَم أَكْمَلُ مِنْ هَدْيِهِ وَأَنَّ حُكْمَ غَيْرِهِ أَحْسَنُ مِنْ حُكْمِهِ كَالذِينَ يُفَضِّلُونَ حُكْمَ الطَّوَاغِيتِ عَلَى حُكْمِهِ فَهُوَ كَافِرٌ.

Nne:  Mwenye kuitakidi kwamba mwongozo wa asiyekuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ndio mwongozo uliokamilika kuliko mwongozo wake, na kwamba hukmu ya asiyekuwa yeye ni hukmu bora kuliko hukmu yake kama wanaofadhilisha hukmu za twaghuti juu ya hukmu zake, basi yeye ni kafiri.

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu [An-Nisaa: 65]

 الخَامِسُ: مَنْ أَبْغَضَ شَيْئًا مِمَّا جَاءَ بِهِ الرَّسُولُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَم وَلَوْ عَمِلَ بِهِ، كَفَرَ

Tano: Anayechukia kitu ambacho amekuja nacho Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) japokuwa atakitekeleza basi yeye ni kafiri.

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ ﴿٨﴾

Na wale waliokufuru, basi ni maangamizo kwao, na Atapoteza ‘amali zao.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ ﴿٩﴾

Hivyo kwa sababu wao wamekirihika ambayo Ameteremsha Allaah, basi Amezibatilisha ‘amali zao. [Muhammad 47: 8-9-]

السَّادِسُ: مَنِ اسْتَهْزَأَ بِشَيْءٍ مِنْ دِينِ الرَّسُولِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَم، أَوْ ثَوَابَ اللهِ، أَوْ عِقَابِهِ، كَفَرَ.

Sita: Atakayefanya istihzai kwa kitu chochote katika Dini ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au akafanya utani katika thawabu au katika adhabu za Allaah, amekufuru.

 

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

يَحْذَرُ الْمُنَافِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلِ اسْتَهْزِئُوا إِنَّ اللَّـهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ ﴿٦٤﴾

Wanafiki wanatahadhari isije kuteremshwa Suwrah itakayowajulisha yaliyomo nyoyoni mwao. Sema: “Fanyeni istihzai; hakika Allaah Atayatoa yale mnayotahadhari nayo.”

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦٥﴾

Na ukiwauliza, bila shaka watasema: “Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?” [At-Tawbah 9: 64-65] 

 السَّابِعُ  : السِّحْرُ وَمِنْهُ: الصَّرْفُ وَالعَطْفُفَمَنْ فَعَلَهُ أَوْ رَضِيَ بِهِ كَفَرَ.

Saba:  Uchawi, na miongoni mwayo ni uchawi wa kutegnanisha na kupendanisha. Basi atakayefanya huo uchawi na akaridhia nayo, amekufuru.

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾

Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua. [Al-Baqarah: 102]

الثَّامِنُ: مُظَاهَرَةُ المُشْرِكِينَ، وَمُعَاوَنَتُهُمْ عَلَى المُسْلِمِينَ.

Nane: Kusaidiana pamoja na washirikina na kushirikiana nao dhidi ya Waislamu.

 

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili kauli Yake Ta’aalaa:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾

Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu. [Al-Maaidah: 51]

 

التَّاسِعُ: مَنْ اعْتَقَدَ أَنَّ بَعْضَ النَّاسِ يَسَعُهُ الخُرُوجُ عَنْ شَرِيعَةِ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَم كَمَا وَسِعَ الخَضِرُ الخُرُوجَ عَنْ شَرِيعَةِ مُوسَى عَلَيهِ السَّلَامُ، فَهُوَ كَافِرٌ.  

Tisa: Mwenye kuitakidi kwamba baadhi ya watu wanaweza kuwa huru kutokutekeleza Shariy’ah ya Muhammad Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyoruhusiwa Al-Khidhr kuwa huru na Shariy’ah ya Muwsaa basi mtu hiyo ni kafiri.

 

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika [Aal-‘Imraan: 85]

 

العَاشِرُ: الإِعْرَاضُ عَنْ دِينِ اللهِ تَعَالَى لَا يَتَعَلَّمُـهُ وَلَا يَعْمَـلُ بِهِ،

Kumi:  Kuikengeuka Dini ya Allaah Ta’aalaa, akawa hajifunzi chochote humo wala hafanyii kazi lolote.

وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:

Na dalili na kauli Yake Ta’’aalaa: 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ ﴿٢٢﴾

Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayaat za Rabb wake, kisha akazikengeukia? Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu. [As-Sajdah: 22]

 

مَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ﴿٣﴾

Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na muda maalumu uliokadiriwa. Na wale waliokufuru kwa yale wanayoonywa kwayo ni wenye kukengeuka.  [Al-Ahqaaf: 3]

وَلَا فَرْقَ فِي جَمِيعِ هَذِهِ النَّوَاقِضِ بَيْنَ الهَازِلِ وَالجَادِّ وَالخَائِفِ إِلَّا المُكْرَهِ.

Na wala hakuna tofauti katika mambo haya yanayomtoa mtu nje ya Uislamu kwa yule anayefanya utani na anayefanya kwa kweli au anayeogopa isipokuwa ambaye amefanya kwa kukirihika kutokana na kulazimishwa kwa nguvu.

وَكُلُّهَا مِنْ أَعْظَمِ مَا يَكُونُ خَطَرًا، وَأَكْثَرِ مَا يَكُونُ وُقُوعًا، فَيَنْبَغِي لِلْمُسْلِمِ أَنْ يَحْذَرَهَا وَيَخَافَ مِنْهَا عَلَى نَفْسِهِ.

Na yote ni hayo ni katika mambo makubwa mno ya khatari  na ambayo yanatokea sana kwa hiyo inampasa Muislamu ajitahadhari nayo na ayakhofie nafsi yake.

نَعُوذُ بِاللهِ مِنْ مُوجِبَاتِ غَضَبِهِ، وَأَلِيمِ عِقَابِهِ.

Tunajikinga kwa Allaah kutokana na yanayopelekea ghadhabu Zake, na adhabu Zake kali.

وَصَلَّى اللهُ عَلَى خَيْرِ خَلْقِهِ مُحَمَّدٍ، وَعَلَى آلِهِ وَصَحْبِهِ وَسَلَّمَ .

Wa Swalla Allaahu ‘alaa khayri Khalqihi Muhammad wa ‘aala aalihi wa Swahbihi wasallam.

 

 

 

 

Share