Nilipotoka Lakini Nimetubu Je Allaah Atapokea Du'aa Zangu? Vipi Kumkwepa Shaytwaan?

 

 

SWALI:

Asalam Alaykum

Thank you for making this good website

 I have  some qustioned that i would like to get the answer for them.
I,am a girl at the age of 18 before i came to europe i was a very good girl but then after settle down in europe i got some friend who was very bad and i used to go with her I became bad as well  I was not wearing the hijjab and not even pray ,but now i returned to god  I thank god for put me in sence and make me realise that the person I was going with she was not good  and my qustion  will god hear my prayers and maybe answer them?  

My second qustion is can i do to get far from shaytan

Thabk you hope i will get answer soon

May god blees you

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Tunashukuru kuona dada zetu wadogo kama wewe umejirudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kupotoka. Hii neema kwako kwani si aghlabu kwa vijana kutumbukia katika madhambi kisha waweze kujirudi haraka hivyo. Wengi wao wanaendelea katika maasi hadi wanafikia umri mkubwa ndipo wanapotanabahi na kurudi. Hao hawakufikiria kuwa mauti yangeliweza kuwafikia wakati bado wako katika maasi. Hivyo ni neema kwako kama ulivyosema umewahi kujizindua. Basi mshukuru sana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kukutoa katika kiza na Akakupa uongofu.

 Kukosea, kufanya dhambi ni jambo la kiasili kwa binaadamu, kwani hakuna aliyekuwa kakamilika. Mtume wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelezea hivyo katika kauli ifuatayo:

  عن أنس رضي الله عنه ((كل ابن آدم خطّاء وخير الخطائين التوابون))  رواه أحمد

Kutoka kwa Anas (Radhiya Allahu 'anhu) ((Kila binaadamu ni mkosa na wakosa bora kabisa ni wanaotubu)) [Imesimuliwa na Ahmad]

Hata kama mtu atafanya madhambi makubwa vipi madam tu atarudi kwa Mola wake, basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atapokea tu tawbah yake na kumsamehe yote ya yaliyopita.

Mfano katika Hadiyth wa mtu aliyeua watu mia kisha akasamehewa:

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : )) كان فيمن كان قبلكم رجل قتل تسعة وتسعين نفسا ، فسأل عن أعلم أهل الأرض ، فدُلَّ على راهب ، فأتاه فقال : إنه قتل تسعة وتسعين نفسا ، فهل له من توبة ، فقال : لا ، فقتله فكمل به مائة ، ثم سأل عن أعلم أهل الأرض ، فدُلَّ على رجل عالم ، فقال : إنه قتل مائة نفس ، فهل له من توبة،  فقال : نعم ، ومن يحول بينه وبين التوبة ، انطلق إلى أرض كذا وكذا ، فإن بها أناسا يعبدون الله ، فاعبد الله معهم ، ولا ترجع إلى أرضك ، فإنها أرض سوء ، فانطلق حتى إذا نصَفَ الطريق أتاه الموت ، فاختصمت فيه ملائكة الرحمة وملائكة العذاب ، فقالت ملائكة الرحمة : جاء تائبا مقبلا بقلبه إلى الله ، وقالت ملائكة العذاب : إنه لم يعمل خيرا قط ، فأتاهم ملَكٌ في صورة آدمي ، فجعلوه بينهم ، فقال : قيسوا ما بين الأرضين ، فإلى أيتهما كان أدنى فهو له ، فقاسوه فوجدوه أدنى إلى الأرض التي أراد ، فقبضته ملائكة الرحمة))  (الإمام مسلم في صحيحه)  .  

Imetoka kwa Abu Sa'iydil-Khudriyyi (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Alikuweko mtu kabla yenu aliua nafsi tisiini na tisa. Akauliza kutaka kumjua aliyekuwa na elimu kuliko wote duniani, akapelekwa kwa mtawa. Akawambia kuwa ameua watu tisini na tisa kisha akamuuliza kama atasamehewa. Mtawa akamwambia "husamehewi". Akamuua na yeye pia ikawa ni watu mia aliowaua.

Akauliza tena kutaka kujua mtu mwenye elimu kabisa duniani akapelekwa kwa mtaalamu. Akamwambia kuwa ameua watu mia na akamuuliza kama atasamehewa. Mtaalamu akamwambia. "Ndio, kwani nani atakayejiweka  baina yako na baina ya tawbah? Nenda mji fulani kwani huko kuna watu wanaomuabudu Allah. Nenda ukaabudu pamoja nao na usirudi mji wako kwani ni mji mbaya huo".

Akaelekea huko lakini alipofika nusu njia Malaika wa kutoa roho akachukua roho yake. Malaika wa Rahma na Malaika wa adhabu wakaanza kumgombania. Malaika wa Rahma akasema: "Ametubu na amekuja kumtafuta Allah". Malaika wa adhabu akasema: "Hakufanya lolote jema". Akatokea Malaika katika umbo la binaadamu akawajia na wakamuomba awahukumie jambo hilo. Akasema: "Pimeni umbali baina ya miji miwili (yaani mji wake aliotoka na mji aliokuwa anaelekea) na wowote utakaokuwa ni karibu zaidi basi ndio huo utakaokuwa ni wake". Wakapima na kuona kwamba mji ambao alikuwa anaelekea kwenda ulikuwa karibu zaidi. Hivyo Malaika wa Rahma akamchukua [Muslim]

[Kwenye As-Swahiyh imesema: "Mji mwema ulikuwa karibu kwa dhiraa moja. Hivyo akahesabiwa kuwa ni mtu wa mji huo"]. [Riwaya nyingine katika As-Swahiyh inasema: "Allah Aliamrisha (mji muovu) usogee mbali hivyo (mji mwema) ukasogea karibu na akasema" Pimeni umbali baina yao" Walipopima waliona kwamba yuko karibu na mji mwema kwa umbali wa dhiraa moja, kwa hiyo akasamehewa]

Kwa hiyo bila shaka madam umetubu, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atakukubalia tawbah yako madamu humshirikishi na kitu chochote na utatia nia kutorudia tena maovu, bila shaka utasamehewa. Na inshaAllaah du'aa zako zitakubaliwa.

Kwa maelezo zaidi bonyeza katika kiungo kifuatacho upate kusoma jinsi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anavyompenda mja wake mwenye kutubia:

Alllaah Anamepnda Mja Anayeomba Tawbah

Swali lako la pili kuhusu kujiepusha na shaytwaan, bonyeza kiungo kifuatacho utapata maelezo kamili na faida zaidi:  

Nataka Kutubu Lakini Shaytwaan kanivaa, Nifanye nini? 

Na Allah Anajua zaidi

 

Share