Kuwatambulisha Watoto Bila DNA

Kuwatambulisha Watoto Bila DNA

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

  

 

Salaam aleikum sheikhe. Swali yangu ni katika dina kama mama wawili wamechanganisha watoto wachanga na kila mama anadai amezaa mtoto mvulana. Je dini inaweza kuwatowanishaje ukiondoa kuchukuliwa DNA. Naomba unijibu kutokana kwa Quran na Sunna.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hukubainisha utata huo ulitokeaje? Ikiwa watoto hao wamezaliwa na kina mama wakawaona watoto wao, basi tatizo hilo  halitakuwepo. Lakini ikiwa wamezaliwa na hao wamama wakawa hawajawaona hao Watoto, ndio tatizo hilo litakuwepo.

 

 

Hadiyth ifuatayo imetaja kuweko ujuzi wa kutambulisha Watoto ni wa nani ulikuweko kabla ya Uislaam:

 

قَالَ يَحْيَى بْنُ سُلَيْمَانَ حَدَّثَنَا ابْنُ وَهْبٍ، عَنْ يُونُسَ،‏.‏ حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا عَنْبَسَةُ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ بْنُ الزُّبَيْرِ، أَنَّ عَائِشَةَ، زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم أَخْبَرَتْهُ أَنَّ النِّكَاحَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ كَانَ عَلَى أَرْبَعَةِ أَنْحَاءٍ فَنِكَاحٌ مِنْهَا نِكَاحُ النَّاسِ الْيَوْمَ، يَخْطُبُ الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ وَلِيَّتَهُ أَوِ ابْنَتَهُ، فَيُصْدِقُهَا ثُمَّ يَنْكِحُهَا، وَنِكَاحٌ آخَرُ كَانَ الرَّجُلُ يَقُولُ لاِمْرَأَتِهِ إِذَا طَهُرَتْ مِنْ طَمْثِهَا أَرْسِلِي إِلَى فُلاَنٍ فَاسْتَبْضِعِي مِنْهُ‏.‏ وَيَعْتَزِلُهَا زَوْجُهَا، وَلاَ يَمَسُّهَا أَبَدًا، حَتَّى يَتَبَيَّنَ حَمْلُهَا مِنْ ذَلِكَ الرَّجُلِ الَّذِي تَسْتَبْضِعُ مِنْهُ، فَإِذَا تَبَيَّنَ حَمْلُهَا أَصَابَهَا زَوْجُهَا إِذَا أَحَبَّ، وَإِنَّمَا يَفْعَلُ ذَلِكَ رَغْبَةً فِي نَجَابَةِ الْوَلَدِ، فَكَانَ هَذَا النِّكَاحُ نِكَاحَ الاِسْتِبْضَاعِ، وَنِكَاحٌ آخَرُ يَجْتَمِعُ الرَّهْطُ مَا دُونَ الْعَشَرَةِ فَيَدْخُلُونَ عَلَى الْمَرْأَةِ كُلُّهُمْ يُصِيبُهَا‏.‏ فَإِذَا حَمَلَتْ وَوَضَعَتْ، وَمَرَّ عَلَيْهَا لَيَالِيَ بَعْدَ أَنْ تَضَعَ حَمْلَهَا، أَرْسَلَتْ إِلَيْهِمْ فَلَمْ يَسْتَطِعْ رَجُلٌ مِنْهُمْ أَنْ يَمْتَنِعَ حَتَّى يَجْتَمِعُوا عِنْدَهَا تَقُولُ لَهُمْ قَدْ عَرَفْتُمُ الَّذِي كَانَ مِنْ أَمْرِكُمْ، وَقَدْ وَلَدْتُ فَهُوَ ابْنُكَ يَا فُلاَنُ‏.‏ تُسَمِّي مَنْ أَحَبَّتْ بِاسْمِهِ، فَيَلْحَقُ بِهِ وَلَدُهَا، لاَ يَسْتَطِيعُ أَنْ يَمْتَنِعَ بِهِ الرَّجُلُ‏.‏ وَنِكَاحُ الرَّابِعِ يَجْتَمِعُ النَّاسُ الْكَثِيرُ فَيَدْخُلُونَ عَلَى الْمَرْأَةِ لاَ تَمْتَنِعُ مِمَّنْ جَاءَهَا وَهُنَّ الْبَغَايَا كُنَّ يَنْصِبْنَ عَلَى أَبْوَابِهِنَّ رَايَاتٍ تَكُونُ عَلَمًا فَمَنْ أَرَادَهُنَّ دَخَلَ عَلَيْهِنَّ، فَإِذَا حَمَلَتْ إِحْدَاهُنَّ وَوَضَعَتْ حَمْلَهَا جُمِعُوا لَهَا وَدَعَوْا لَهُمُ الْقَافَةَ ثُمَّ أَلْحَقُوا وَلَدَهَا بِالَّذِي يَرَوْنَ فَالْتَاطَ بِهِ، وَدُعِيَ ابْنَهُ لاَ يَمْتَنِعُ مِنْ ذَلِكَ، فَلَمَّا بُعِثَ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم بِالْحَقِّ هَدَمَ نِكَاحَ الْجَاهِلِيَّةِ كُلَّهُ، إِلاَّ نِكَاحَ النَّاسِ الْيَوْمَ‏.‏

 

Imepokewa kwa ‘Urwah bin az-Zubayr kuwa ‘Aaishah, mkewe Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amempasha khabari kuwa kulikuwa na ndoa aina nne katika ujaahiliyyah. (Kabla ya Uislaam)    

 

Aina ya kwanza: Mwanamme alikuwa akiposa msichana kwa mlezi wake au akiposa binti yake, na akimpatia mahari, kisha kumuoa (ndoa kama ilivyo sasa).

 

Aina ya pili: Alikuwa mume akimwambia mkewe pindi anapojitwahirisha baada ya hedhi yake: “Nenda kamuite fulani na mfanye jimai naye”. Mumewe baada ya hapo atajitenga naye wala hatolala naye mpaka atakapopata uja uzito wa yule mwanamme mwingine aliyelala naye. Pindi uja uzito wake unapokuwa umebainika, mumewe atalala naye akitaka. Mumewe alifanya hivyo (yaani kumuacha mkewe kulala na mwanamme mwingine) ili apate kutoka kwake mtoto mtukufu. Ndoa aina hizo zilikuwa zikiitwa al-Istibdhwaa‘.

 

Aina ya tatu: Wanakusanyika kikundi cha watu wasiozidi kumi na kumuingilia mwanamke mmoja na wote watafanya jimai naye. Pindi atakapopata uja uzito na kuzaa mtoto na baada siku chache kupita baada ya kuzaa kwake, alikuwa akituma ujumbe kwa wote kujumuika na hakuna hata mmoja aliyekataa mwito huo wa kuja. Na wote wanakusanyika mbele yake, alikuwa akiwaambia, “Nyote mwajua mlichofanya na sasa nimejifungua mtoto. Kwa hiyo, huyu ni mtoto wako ee fulani”. Akamtaja anayempenda na huyo mtoto atamfuata yeye wala hatakataa kumchukua.

 

Aina ya nne ni:  Walikuwa wakikusanyika watu wengi, wakimuingilia mwanamke mmoja wala (huyo mwanamke) hakumkataa aliyekuja kwake. Hawa ni wale malaya waliokuwa wakiweka bendera milangoni mwao kama ishara, na mwanamme yeyote anayetaka alikuwa anaweza kuja kufanya jimai nao. Yeyote miongoni mwao aliyepata uja uzito na kuzaa, wanaume wote walikuwa wakikusanywa kwa ajili yake na kumuita Qaafah (watu waliokuwa mahiri katika kumfananisha mtoto na mzazi wake) kwao na walikuwa wakimuacha mtoto amfuate mwanamme (waliomtambua kuwa ndiye baba). Na mwanamke alikuwa akimuachia awe naye na vilevile kuitwa mtoto wake. Mwanamme huyo alikuwa hawezi kukataa yote hayo. Pindi alipotumilizwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa haki na ukweli alivunja (aliziondoa) ndoa zote za kijaahiliya isipokuwa ndoa ile inayofanywa na watu leo (yaani ndoa aina ya kwanza) [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Nikaah]

 

 

Ujuzi huo uliotajwa katika aina nne ya ndoa za kijaalihiliyyah, wa kutambulisha Watoto ni wa nani,  upo mpaka wakati wetu wa leo. Wapo watu wakimuona tu mtoto  kuwa mtoto anafana na baba au mama. Wakati mwengine anakufahamisha mdomo huu ni kama wa babu yake, pua ni kama ya mama, macho yake ni kama shangazi yake na mfano wake.

 

 

Ikiwa tatizo hilo lipo basi mjuzi wa aina hiyo anaweza kutatua tatizo hilo mara moja bila ya kuendea njia za kisasa za kutumia DNA (deoxyribonucleic acid) [DNA ni kitu (molekyuli) cha kiini ya seli ambacho kinakuwa na maelezo ya kijenetiki (vinasaba), inatambua muundo, utendaji na tabia ya seli]

 

 

Na ikiwa mjuzi hakupatikana, basi njia hiyo ya kisayansi inakubalika ki-Shariy’ah na kwa maelezo bayana bonyeza kiungo kifuatacho:

 

DNA Katika Uislaam Nini Hukmu Yake?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share