08-Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiy: Mwanamke Anayelazimishwa Kujimai Wakati Wa Ramadhwaan

Mwanamke Anayelazimishwa Kujimai Wakati Wa Ramadhwaan

 

Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiy

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ikiwa mwanamke atalazimishwa jimai, halazimiki kulipa kafara, bali analazimika kulipa  tu siku hiyo?

 

JIBU:

 

 Muhannaa kasema:  "Nilimuuliza Ahmad kama mwanamke aliyebakwa analazimika kulipa siku hiyo.  Akasema: "Ndiyo." Pia nikamuuliza kama analazimika kulipa kafara, akasema: "Hapana!"

 

Maoni haya anakubaliana nayo pia al-Hasan, Ath-Thawriy, Al-Awza'iy na Hanafiyyah. 

 

Kulingana na swali hili, inamuhusu pia mwanamke ambaye kaingiliwa wakati amelala.

 

Maalik kasema kuhusiana na mwanamke aliyelala: "Ni juu yake kulipa siku hiyo, ila hatolipa kafara. Ama kuhusiana na mwanamke ambaye amelazimishwa kujimai, analazimika kulipa siku hiyo na kutoa kafara.”

 

Ash-Shaafi'iy, Abuu Ath-Thawriy na Ibnul-Mundhir wanasema ikiwa ataingiliwa jimai  kwa matisho, basi wana maoni sawa na sisi.

 

[Al-Mughniy (4/376) Daar 'Alaam-il-kutub, 1419/1999]

 

 

 

Share