Skip to main content

Fataawaa: Kukithirisha 'Ibaadah Na 'Amali Ramadhwaan01-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Ipi Bora Kusoma Qur-aan Au Tafsiyr Katika I`tikaaf?

Ipi Bora Kusoma Qur-aan Au Tafsiyr Katika I`tikaaf?

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan

www.alhidaaya.com

SWALI:

 

Ipi bora kwa mwenye kukaa I´tikaaf, kusoma Qur-aan tu au kusoma Tafsiyr na kuizingatia? 

JIBU:

Kusoma Qur-aan ni bora zaidi kwa kuwa kisomo chake kina fadhila katika Ramadhwaan kuliko (miezi mengine). Ama kusoma tafsiri anaweza kufanya hilo wakati mwingine si katika hali ya I´tikaaf. Usomaji wa Qur-aan ubora wake ni wakati wa I´tikaaf, na kujishughulisha kwake kusoma Qur-aan huku anahifadhi ni bora zaidi kuliko kusoma Tafsiyr. 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy - Shaykh Swaalih Al-Fawzaan]