03-Imaam Ibn Baaz: Lipi Bora Kufanya Katika Mchana Wa Ramadhwaan; Kusoma Qur-aan Au Kuswali Sunnah

Lipi Bora Kufanya Katika Mchana Wa Ramadhwaan; Kusoma Qur-aan Au Kuswali Sunnah

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Kitendo gani bora kufanya katika siku za Ramadhaan, kusoma Qur'aan au kuswali Swalah za Sunnah?

 

 

JIBU:

 

Ilikuwa ni mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni kufanya aina nyingi ‘ibaadah katika Ramadhaan.  Jibriyl alikuwa akimsomesha Qur-aan wakati wa usiku.  Na Jibriyl alipokutana naye alikuwa mkarimu katika swadaqah kuliko upepo unaovuma.  Alikuwa ni mtu mkarimu kabisa kuliko wote na alikuwa zaidi mkarimu katika mwezi wa Ramadhaan.

Wakati huu wa Ramadhaan alikuwa akitoa swadaqah zaidi na alikuwa akifanya ihsaan kwa watu, akisoma Qur-aan zaidi, akiswali zaidi, akifanya dhikir na akikaa I'tkaaf.  

Huu ndio mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika maudhui hii na katika mwezi huu mtukufu.

 

Kuhusu kitendo gani bora kufanya kusoma Qur-aan au kuswali zaidi, inatofautiana kutokana na hali ya mtu na uwezo huo unarudi kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) kwani Yeye ni Mwenye kuzunguka kila kitu (kwa ujuzi Wake).  

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy – Imaam Ibn Baaz]

 

 

Share