09-Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiyy: Mwanaume Ambaye Kalazimishwa Kujima Na Mkewe Katika Ramadhwaan

Mwanaume Ambaye Kalazimishwa Kujima Na Mkewe Katika Ramadhwaan

 

Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiyy (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Ikiwa mwanaume atalazimishwa kujimai, basi  Swawm yake inabatilika, na pia Swawm ya mwanamke inavunjinka kwa sababu ya jimai. Swawm ya mwanaume ni aula zaidi kubatilika kwa sababu hiyo hiyo.

 

Kuhusiana na kafara anasema Al-Qaadhwiy:

 

"Ni waajib kwake kulipa kafara, kwa sababu haiwezekani (kwa mwanaume) kalazimishwa jimai. Mwanaume hawezi kufanya jimai bila kwanza ya dhakari yake kusimama, na dhakari kusimama inasababishwa na matamanio. Kwa hali hiyo haonelei kabisa kuwa (mwanaume) alilazimishwa.

 

Abul-Khattwaab anasema: "Kuna mapokezi mawili. Moja inasema kuwa si lazima kwake kulipa kafara."

 

Hii pia ni kauli ya Ash-Shaafi'iy. Suala zima la kafara ni ili imtakase mtu kwa madhambi yake. Kwa hivyo haihusiani na mtu kulazimishwa, kwa kuwa mtu anakuwa hana makosa. Hata hivyo anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 

"Ummah wangu umesamehewa makosa ya mtu kusahau na kulazimishwa."

 

Vile vile Shariy'ah haijataja kuwa analazimika kutoa kafara.”

 

Ibn ‘Aqiyl kasema mwanaume ambaye amelala (huku) dhakari yake imesimama, mke wake akaiingiza tupu wake kwake (kwa mumewe aliyelala): "Hatalazimika kulipa siku hiyo wala kulipa kafara”

 

 

[Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiyy - Al-Mughniy (4/377)]

 

 

Share