Makaroni Ya Kamba Na Kusa Kwa Sosi Nyeupe Ya Cream

Makaroni Ya Kamba Na Kusa Kwa Sosi Nyeupe Ya Cream

 

Vipimo 

Makaroni kiasi 250 gms

Kamba saizi kubwa kiasi  ½ kilo

Kusa (Zuchini/mumunya dogodogo la kijani) 2

Kitunguu 1 katakata

Nyanya 1 katakata

Chumvi kiasi

Pilipili manga ½ kijiko cha chai

Cream ya kupikia (Cooking cream) ½ kikombe

Maziwa vijiko 2 vya kulia

Parsely (kotmiri mwitu)

Mafuta  ya zaytuni ¼ kikombe

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Chemsha makaroni katika maji ya moto dakika 10 kisha epua uchuje maji weka kidonge cha siagi ukoroge yasigande.
  2. Safisha na osha kamba uchuje maji.
  3. Katakata kusa/zucchini slice za duara.
  4. Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu vilainike.
  5. Tia kusa na nyanya kaanga katika moto mdogo mdogo.
  6. Weka kamba endelea kukaanga.
  7. Tia macaroni, chumvi pilipili changanya vizuri.
  8. Tia cream na maziwa changanya vizuri katika moto kisha epua sufuria upake katika sahani utolee na parsley.

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

Share