Makaroni Na Kuku Wa Tanduri

Makaroni Na Kuku Wa Tanduri 

Vipimo

Makaroni - 500 gms

Vipimo Vya Kuku

Kuku - 3 LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Tanduri masala - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) - 2 vijiko vya supu

Jiyrah (cummin powder) - 1 kijiko cha chai

Dania (coriander powder) - 1 kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Ukwaju - ¼ kikombe

Namna Ya kutayarisha Na Kupika:

  1. Changanya vitu vyote pamoja mroweke kuku kwa muda wa masaa
  2. Mchome (broil) katika oveni au katika jiko la mkaa kama B.B.Q – mweke kando.

Sosi Ya Makaroni

Vitunguu maji viliyokatwa katwa - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Nyanya zilizosagwa - 3

Nyanya kopo - 1 kijiko cha supu

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Oregano - 1 kijiko cha chai

Nanaa iliyokatwa katwa - 2 msongo (bunch)

Chumvi - kiasi

Mafuta - ¼ kikombe

Namna Ya Kutayarisha na Kupika

  1. Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu maji hadi vigeuke rangi.
  2. Tia thomu endelea kukaanga, tia nyanya, nyanya kopo, pilipili manga, oregano, chumvi endelea kukaanga.
  3. Mwisho tia nana koroga sosi ikiwa tayari.
  4. Makaroni Na Namna Ya Kupakua
  5. Chemsha makoroni hadi yaive  yachuje kwa kumwaga maji.
  6. Pakuwa macaroni katika sahani au chombo na mwagia sosi juu yake kisha kuku, na tolea  na saladi au mapilipili mboga.

  

 

 

Share