Shurba Ya Kuku Na Oats Iliyokobolewa - 1

Shurba Ya Kuku Na Oats Iliyokobolewa  - `

 

Vipimo

Kuku nusu

Ngano zilokobolewa (jariysh/cracked oats) kikombe 1 ½

Kitunguu 1 katakata

Pilipili manga kijiko 1 cha chai

Nyanya 1 ilosagwa

Kidonge cha supu (ukipenda)

Chumvi

Siki ya zabibu vijiko 2 vya kulia

Mafuta vijiko 3 vya kulia

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Roweka jariysh (oats ngano zilokobolewa) katika maji kiasi kwenye bakuli.
  2. Katakata kuku umchemshe kwa chumvi na pilipili manga achemke na abakie supu yake.
  3. Epua umchambue chambue kuku utoe mifupa  weka kando.
  4. Kaanga kitunguu ulichokikatakata kidogo kidogo mpaka kilainike, tia nyanya kaanga kidogo.
  5. Mimina supu na ukipenda weka kidonge cha supu. Ikichemka tia  ngano ulizoroweka na maji yake. Acha ichemke kidogo ziive.
  6. Mimina kuku, tia siki uonje chumvi, mimi kama katika bakuli ikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

Share