Shurba Ya Nyama Ng’ombe Na Oats Zilokobolewa -1

Shurba Ya Nyama Ng'ombe Na Oats Ilokobolewa -1

 

Vipimo 

 

Nyama ng’ombe ya mifupa kilo 1

Tangawizi na thomu (garlic/saumu) ilosagwa vijiko 2 vya kulia

Mdalasini kijiti 1

Oats ilokobolewa (quacker oats) kikombe 1 ½

Kitunguu katakata

Samli kiasi vijiko 3 vya kulia

Nyanya katakata

Kidonge cha supu 1

Kotmiri katakata msongo (bunch) 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Chumvi kisia

Ndimu au siki vijiko 3 vya kulia

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Chemsha nyama kwa chumvi na pilipili manga, tangawizi na thomu, mdalasini. Weka maji ya kutosha ili yabakie kama supu. Acha iwive vizuri kabsia ilainike sana kiasi ya kuwa inachambuka chambuka. Chemsha katika pressure cooker ikiwa unalo.
  2. Epua toa nyama uchambe chambue, ikiwa haikuwiva basi itie katika mashine ya kukatakata (chopper) uashe kidogo ivurugike.
  3. Weka samli katika sufuria, tia vitunguu ukaange mpaka ianze kugeuka kuwa rangi ya hudhurungi.
  4. Weka nyanya kaanga kidogo.
  5. Mimina supu na kidonge cha supu kisha tia oats zichemke.
  6. Mwisho kabisa weka kotmiri, siki au ndimu kidogo, onja chumvi epua ikiwa tayari.

 

 

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share