Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Sharh Thawabu Za Kumfuturisha Mwenye Swawm

 

Sharh Thawabu Za Kumfuturisha Mwenye Swawm

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kuhusu Hadiyth Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((Atakayemfuturisha Aliye Na Swawm Atapata Thawabu Kama Zake Bila Ya Mwenye Swawm Kupungukiwa Na Kitu)).

 

Wamekhitilafiana ‘Ulamaa katika maana ya “Atakayemfuturisha mwenye swawm.” Ikasemwa: Lilokusudiwa kumfuturisha ni chochote kidogo anochofuturu japo kama ni tende. Na wengine wakasema: Imekusudiwa amfuturishe kwa kumshibisha kwa sababu ndio itakayomsaidia mwenye swawm usiku wake wote na huenda ikamtosheleza na sahuwr (daku). Lakini iliyo dhahiri katika Hadiyth ni kwamba mtu akimfuturisha mwenye swawm japo kwa tende moja basi atapata thawabu sawa na thawabu zake.  Kwa hiyo basi inampasa mtu atilie himma kufuturisha wenye swawm kwa kadiri ya uwezo wao khasa kwa vile wenye swawm wanahitaji kusaidiwa kutokana na umasikini wao na kuhitaji kwao kwa vile hawapati wenye kuwaandalia futari na kama hayo.

 

 

[Imaam Ibn 'Uthaymiyn – Sharh Riyaadhw Asw-Swaalihiyn]

 

 

Share