13-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Taraawiyh Au Qiyaam Kuswali Baada Ya 'Ishaa Na Usiku Katika Makumi Ya Mwisho

Taraawiyh Au Qiyaam Kuswali Baada Ya 'Ishaa Na Usiku

Katika Makumi Ya Mwisho

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan, Waislamu huongeza juhudi katika ‘ibaadah wakifuata muongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuitafuta Laylatul-Qadr ambayo ni bora kuliko miezi elfu.

 

Wanaoswali rakaa ishirini na tatu mwanzo wa mwezi, huzigawa Swalaah katika masiku kumi ya mwisho ili waswali rakaa kumi mwanzo wa usiku (baada ya ‘Ishaa) ambayo inaitwa Taraawiyh. Kisha huswali kumi zingine usiku wa manane, huku wakizirefusha na kufuatilia rakaa tatu za Witr ambazo wanaziita (hiyo Swalaah ya usiku wa manane) ni Qiyaam.

 

Hayo majina ya Swalaah hizo ni kuzitofautisha tu. Lakini ukweli ni kwamba zote zinaweza kuitwa Taraawiyh au kuitwa Qiyaam.

 

Ama wale wanaoswali rakaa kumi na moja au kumi na tatu mwanzo wa usiku, huzidisha rakaa kumi katika masiku kumi ya mwisho ambayo huswali usiku wa manane, huku wakizirefusha na kutafuta fadhila za masiku kumi ya mwisho kwa kuongeza juhudi kufanya mema, kwa kufuata waliotangulia katika Maswahaba na wengineo walioswali rakaa ishirini na tatu kama ilivyotajwa juu. Hivyo basi wanajumuisha rai mbili; Rai yenye kupendekeza kuswali rakaa kumi na tatu katika masiku ishirini ya mwanzo. Na Rai yenye kupendekeza kuswali rakaa ishirini na tatu katika masiku kumi ya mwisho.

 

 

[It-haaf Ahlil-Iymaan bi Majaalisi Shahri Ramadhwaan]

 

 

Share