06-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Swawm Za Sita Za Shawwaal Zikiangukia Jumatatu Na Alkhamiys Kunapatikana Thawabu Kwa Zote?

Swawm Ya Siku Sita Za Shawwaal Zikiangukia Jumatatu Na Alkhamiys Kunapatikana Thawabu Kwa Zote Ikiwekwa Niyyah Mbili

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

"Inapoafikiana kuwa Swawm katika masiku haya sita (siku sita za mwezi wa Shawwaal) na (yakukutana) na siku ya Jumatatu au Alkhamiys, basi (mtu) hupata ujira wa (Swawm) mbili (anapofunga) kwa niyyah  ya (kupata) ujira wa masiku sita (ya Shawwaal) na kwa niyyah ya (kupata) ujira wa siku ya Jumatatu au Alkhamiys, kwa kauli yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"Hakika matendo (hulipwa) kwa niyyah, na hakika kila mtu (hulipwa) kwa kile alichonuia."

 

 

[Fataawaa Islaamiyyah, mj. 2, uk. 154]

 

 

Share