Iyd Al-Fitwr: Yaliyo Sunnah Kutekelezwa

 

'Iyd Al-Fitwr: Yaliyo Sunnah Kutekelezwa

 

Alhidaaya.com

 

 

Ni siku ya kumalizika Swawm na siku ya kula, kunywa na kufurahi kwa kila aina ya furaha yenye kukubalika kishariy’ah na pia kuwafurahisha watoto wahisi kuwa ni sikukuu yao kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((إن لكل قوم عيداً، وهذا عيدنا)) البخاري و مسلم

((Kwa kila kaumu (jamii ya watu) kuna sikukuu, na hii (‘Iyd) ndiyo sikukuu yetu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Yafuatayo Ni Sunnah Kufanywa Siku Ya 'Iyd:

 

1. Kuvaa Nguo Nzuri Na Vizuri Zaidi Kuvaa Nguo Mpya Ya Halali

 

عن نافع:  "أن ابن عمر رضي الله عنهما كان يغتسل يوم الفطر قبل أن يغدو إلى المصلى" أخرجه مالك - إسناد صحيح

 

 

2. Kwenda Kwenye Swalah Ya ‘Iyd Wote, Hata Wanawake Wenye Hedhi, Watu Wazima Na Watoto

 

وعن أم عطية رضي الله عنها قالت:  "أُمرناأن نَخرج، فنُخرج الحُيَّض والعواتق وذوات الخدور. فأما الحُيَّض فيشهدن جماعة المسلمين ودعوتهم، ويعتزلن مصلاهم " أخرجه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Ummu 'Atwiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: "Ametuamrisha tutoke, wakatoka walio katika hedhi, wazee vikongwe, ama walio katika hedhi wanashuhudia tu Swalah ya Jamaa na khayr na du'aa zake." [kwa kukaa nyuma ya uwanja wa kuswalia Swalah ya ‘Iyd. Ni Sunnah kuswalia ‘Iyd uwanjani na si Msikitini]) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

3. Kula Tende Kabla Ya Kwenda Kuswali Swalah Ya 'Iyd Na Kuila Kwa Witr (Moja, Tatu, Tano n.k.)

 

عن أنس رضي الله عنه قال : " كان النبي صلى الله عليه وسلم لا يغدوا يوم الفطر حتى يأكل تمرات، ويأكلهن وتراً " أخرجه البخاري 

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu ambaye amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki (kwenda kuswali) ila baada ya kula baadhi ya tende na alikuwa akizila kwa witr" [Al-Bukhaariy]

 

 

4. Kuleta Takbira Kwa Sauti

 

عبدالله بن عمر رضي الله عنهما: "أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يكبر يوم الفطر من حيث يخرج من بيته حتى يأتي المصلى"حديث صحيح بشواهده

 وعن نافع: "أن ابن عمر كان إذا غدا يوم الفطر ويوم الأضحى يجهر بالتكبير حتى يأتي المصلى، ثم يكبر حتى يأتي الإمام، فيكبر بتكبيره"  أخرجه الدارقطني وغيره بإسناد صحيح 

Kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema:"Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akileta Takbiyr siku ya Fitwr alipokuwa akitoka nyumbani kwake hadi kufika Muswallaa (Uwanja au eneo lililotengwa kuswalia Swalah ya ‘Iyd)." [Hadiyth Swahiyh]

 

Na kutoka kwa Naafi': "Kwamba Ibn 'Umar alikuwa akitoka siku ya Fitwr na siku ya Adhwhaa akipiga Takbiyr kwa sauti hadi anapofika katika Muswallaa, kisha anaendelea kuleta Takbiyr hadi anapokuja Imaam huleta Takbiyr yake." [Ad-Daaraqutwniy na wengineo kwa isnaad Swahiyh]

 

 

Jinsi Ya Kupigwa Takbira

 

Allaahu Akbar, Allaahu Akbar 

Laa Ilaaha Illa Allaah 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar 

Wa Lillaahil Hamd 

 

  

5. Kwenda Kuswali Kwa Kutembea (Ni Bora Kuliko Kuutumia Kipando Kama Gari Na Vinginevyo)

 

لحديث علي رضي الله عنه قال : "من السنة أن يخرج إلى العيد ماشيا" أخرجه الترمذي، وهو حسن بشواهده

Hadiyth kutoka kwa 'Aliy: "Ni Sunnah kutoka kwenda (kuswali) 'Iyd kwa kutembea." [At-Tirmidhiy nayo ni Hadiyth Hasan]

 

 

6. Kubadilisha Njia Wakati Wa Kwenda Kuswali Na Wakati Wa Kurudi

 

لحديث جابر قال: "كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا كان يوم عيد خالف الطريق"  أخرجه البخاري 

Hadiyth ya Jaabir ambaye amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitofautisha njia" (za kwendea kuswali). [Al-Bukhaariy]

 

 

7. Kuswali Kwenye Muswallaa (Uwanja/Eneo La Kuswalia)

 

 

8. Kuamkiana Na Kutembeleana Kwa Furaha Na Mapenzi. Ni Vizuri Kuamkiana Kama Walivyokuwa Wakiamkiana Maswahaba Kwa Kusema:

تَقَبَّلَ اللَّهُ مِنَّا ومِنْكُمْ

Taqabbala Allaahu Minnaa Wa Minkum

 

 

9. Kuwafurahisha Watoto Kwa Kuwapa Zawadi Ukiweza

 

 

10. Wanawake (Wakiwa Peke Yao) Kupiga Dufu Na Kuimba Nyimbo Zenye Maadili Zisizokuwa Na Muziki

 

 

Tunawaombea 'Iyd yenye khayr na furaha na mapenzi baina ya ndugu, jamaa, marafiki na Waislamu wote kwa ujumla.

 

 

Taqabbala Allaahu Minnaa Wa Minkum

 

Share