17-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Je, Inafaaa Swiyaam Za Sunnah Bila Ya Kutanguliza Niyyah?

Je, Inafaaa Swiyaam Za Sunnah Bila Ya Kutanguliza Niyyah?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

"Ikiwa mtu hakutia niyyah kufunga Swiyaam za Sitta Shawwaal isipokuwa akatia niyyah mchana, basi hatoandikiwa kuwa amefunga siku kamili. Basi akitia niyyah siku ya kwanza wakati wa Adhuhuri, kisha baada ya hapo akafunga siku tano, basi atakuwa hakuzipata siku sita kwa sababu amefunga siku tano na nusu, kwa vile thawabu haziandikwi isipokuwa kwa niyyah kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

“Hakika kusihi kwa ‘amali huzingatiwa na niyyah. Na hakika kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia.”

 

Na hivyo yeye mchana wa siku hiyo hakutia niyyah kufunga kwa hivyo hapati ukamilifu wake.  Naam."

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb, kanda (296)

 

Share