03-Ruqyah: Du’aa Za Sunnah Kwa Ajili Ya Maradhi Na Mabaya Mengineyo

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqya: Du’aa Za Sunnah Kujikinga Na Maradhi Na Mabaya Mengineyo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kupatwa maradhi ni miongoni mwa mitihani ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na inampasa Muumini awe na subra kwa ajili ya kupata radhi za Allaah (‘Azza wa Jalla), pamoja na fadhila zake tele, miongoni mwazo ni kufutiwa madhambi mpaka mtu atakasike nayo.

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ابن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) قَالَ دَخَلْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يُوعَكُ، فَمَسِسْتُهُ بِيَدِي فَقُلْتُ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّكَ لَتُوعَكُ وَعْكًا شَدِيدًا" فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَجَلْ، إِنِّي أُوعَكُ كَمَا يُوعَكُ رَجُلاَنِ مِنْكُمْ)) فَقُلْتُ: "ذَلِكَ أَنَّ لَكَ أَجْرَيْنِ؟"  فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَجَلْ)) ثُمَّ قَالَ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يُصِيبُهُ أَذًى مِنْ مَرَضٍ فَمَا سِوَاهُ إلاَّ حَطَّ اللَّهُ بِهِ سَيِّئَاتِهِ كَمَا تَحُطُّ الشَّجَرَةُ وَرَقَهَا)) متفق عليه

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Niliingia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anaugua homa. Nikamgusa kwa mkono wangu nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika una homa kali?  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ndio! Ninaugua kama wanavyougua wawili wenu)). Nikasema: “Je, ni kwa sababu utapata thawabu mara mbili?”  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ndio)) kisha akasema: ((Hakuna Muislamu yeyote anayefikwa na dhara kutokana na maradhi au vinginevyo isipokuwa Allaah Atamfutia madhambi yake mfano wa majani yanavyopuputika mtini)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida zaidi: 

 

04 - Subira Anaposibiwa Muislamu Na Maradhi

 

Du’aa alizokuwa akiomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kujikinga na maradhi pamoja na masaibu mengineyo:

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْبَرَصِ وَالْجُنُونِ وَالْجُذَامِ وَمِنْ سَيِّئْ الاَسْقَامِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-baraswi wal-junuwni wal-judhaami wamin sayyiil-asqaami

 

(Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na mambalanga na umajnuni, na ukoma na maradhi mabaya)) [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ahmad. Swahiyh katika Swahiyh An-Nasaaiy (3/1116)]

 

 اللَّهُمَّ جَنِّبْنِي مُنْكَرَاتِ الاَخْلاَقِ، وَالاَهْوَاءِ، وَالاَعْمَالِ، والأدْوَاءِ

Allaahumma jannibniy munkaraatil-akhlaaqi, wal ahwaahi, wal-a’maali, wal adwaai

 

Ee Allaah niepushe machukizo ya tabia na matamanio, na matendo (maovu), na maradhi. [Al-Haakim na kasema Swahiyh kwa sharti ya Muslim na ameikubali Adh-Dhahabiy. Kitabus-Sunnah (13)  na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسْلِ والْجُبْنِ وَالْبُخْلِ وَالْهَرَمِ وَالْقَسْوَةِ وَالْغَفْلَةِ وَالْعَيْلَةِ وَالذِّلَّةِ وَالْمَسْكَنَةِ  وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْفَقْرِ وَالْكُفْرِ وَالْفُسُوقِ وَالشِّقَاقِ وَالنِّفَاقِ وَالسُّمْعَةِ وَالرِّياَءِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الصَّمَمِ  وَالْبُكَمِ والْجُنُونِ وَالْجُذَامِ والْبَرَصِ وَسَيِّءِ الاَسْقَامِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-‘ajzi, wal-kasli, wal-jubni, wal-bukhli, wal-harami, wal-qaswati, wal-ghaflati, wal-‘aylati, wadh-dhillati, wal-maskanati, wa a’uwdhu bika minal-faqri, wal-kufri, wal-fusuwqi, wash-shiqaaqi, wan-nifaaqi, wassum-’ati, warriyaai, wa a’uwdhu bika minasw-swamami, wal-bukami, wal-junuwni, wal-judhaami, walbaraswi, wasayyiil-asqaami

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kushindwa nguvu [kutojiweza], na uvivu, na uoga, na ubakhili, na kudhoofika [kutokana na uzee], na  moyo mgumu, na kughafilika, na kufedheheka, na kudhalilika, na umasikini, na najikinga Kwako na ufakiri, na kufru, na ufasiki, na magomvi, na unafiki, na kupenda kusikika umaarufu, na riyaa, na najikinga Kwako dhidi ya uziwi na ububu na ukichaa na ukoma na mbalanga na maradhi mabaya. [Al-Haakim, Al-Bayhaqiy na Taz. Swahiyh Al-Jaami’ (1/406]

 

 

 

 

Share