Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kurudia Kuomba Du’aa Mara Tatu Ni Sunnah?

Kurudia Kuomba Du’aa Mara Tatu Ni Sunnah?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Katika shuruti za du’aa ni kukariri mara tatu. Na khatibu siku ya Ijumaa alisoma na akataja du’aa mara moja baada ya khutbah Msikitini. Je inajuzu hivyo?

 

JIBU:

 

Si sawa hivyo alivyofahamu ndugu huyo kwamba ni sharti ya du’aa kuikariri mara tatu,  bali hivyo ni miongoni mwa adaab (za du’aa) ambayo si  sharti. Na inajuzu mtu amuombe Allaah (Ta’aalaa) mara moja, yaani asikariri ibara anayoitamka, kwani kukariri ni katika adaab na si katika sharti.

 

Lakini muhimu ajue kwamba katika sharti za du’aa ni kwamba mtu aamini kwamba anayemuomba ni  Mweza kwa kumuitikia du’aa yake.  Na kadhalika katika adaab muhimu sana ni kujiepusha na haraam katika kula na kunywa na mavazi, kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja mtu aliyekuwa katika safari ndefu akiwa katika hali ya uchafu na  mavumbi,  amenyanyua mikono yake mbingu akiita: “Yaa Rabb, Yaa Rabb”  na haya yote ni katika sababu za kuitikiwa du’aa.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  (Kuhusu huyo msafiri) “Na hali chakula chake ni haraam na kinywaji chake ni haraam, na mavazi yake ni haraam na amelishwa vya haraam,   basi vipi ataitikiwa?”  Basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaweka mbali kuitikiwa kwa du’aa ya mtu huyo kwa kuweko  ambayo yanazuia kwa nguvu kuitikiwa du’aa, nayo ni kula  kwake haraam na mavazi yake.

 

Ama  kitendo cha Khatibu kwamba amesoma du’aa mara moja wakati khutba yake  basi hakuna ubaya kitendo chake hicho.

 

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb – Sharitw (2)]

 

 

  

Share