Shaykh Fawzaan: Kitabu “Hayaatu Asw-Swahaabah” Cha Kandhlawi Hakifai - Mwanzilishi Wa Jamaa’atu At-Tabliygh

 

Kitabu “Hayaatu Asw-Swahaabah” Cha Kandhlawi (Kandahlawi)

Hakifahi -Mwanzilishi Wa Jamaa’atu At-Tabliygh

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Ni ipi rai yenu enyi wenye fadhila kuhusu kitabu “Hayaatu Asw-Swahaabah”?

 

 

JIBU:

 

Hiki ni kitabu cha Matablighi (Jamaa’atu At-Tabliygh) ambao wanatilia umuhimu (masuala) ya fadhila za matendo (Fadhwaailu Al-A’maal) na wala hawayapi umuhimu (masuala) ya ‘Aqiydah na Tawhiyd.

 

Wanayapa umuhimu mambo ya fadhila za matendo tu! Ni madhehebu ya Kisufi.

 

Na’am… Hawayapi umuhimu (masuala) kuwa Maswahaba walipigana Jihaad kwa ajili ya Allaah, hawayapi umuhimu (masuala) kuwa Maswahaba walijifunza Tawhiyd na wakafanya Ikhlaasw katika ‘Ibaadah.

 

Hawayapi umuhimu mambo hayo bali wanachojali wao kuyapa umuhimu ni mambo ya fadhila za matendo tu!

 

 

[https://safeshare.tv/submit?url=https%3A%2F%2Fwww.youtube.com%2Fwatch%3Fv%3DpxqiMvkcTJk ]

 

 

Share