Kuunga Safu Baina Ya Nguzo

 

SWALI:

na la mwisho kuunga safu baina ya pila ina juzu? Kwa haya machache natumai utanijubu kwa haraka ewe ndugu yangu na wabillahi tawfiq!

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Bila shaka ikiwa tumekufahamu sawasawa kwa neno pila, ambalo ni la Kiingereza Pillar, kwa Kiswahili tunasema nguzo, inakuwa haifai kwani huweza kushikanisha miguu baina ya watu wawili. Ikiwa watu hawajai katika Msikiti basi pale kwenye kiguzo watu hawatapanga mstari au kuunga safu, lakini ikiwa Msikiti unajaa pomoni watu wanaweza kupanga safu sehemu ambayo kipo kiguzo hicho.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share