Taraawiyh: Akiswali Taraawiyh Masjid Inajuzu Aswali Tena Nyumbani Akiamka Usiku?

  

Akiswali Taraawiyh Masjid Inajuzu Aswali Tena Nyumbani Akiamka Usiku?

 

 www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Muislamu akiswali Taraawiyh msikitini, je, Anaruhusiwa na kuswali Swalaah ya usiku nyumbani?  Vipi Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali kwake usiku? 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

 

Muislamu akiswali jama'ah Swalaah ya Taraawiyh Masjid na akitaka kuswali zaidi nyumbani basi aswali mfululizo wa Raka'ah mbili Masjid kisha asiswali huko Witr kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  ((Hakuna Witri mbili kwa usiku mmoja )) [Ahmad na wengineo na imepewa daraja ya Swahiyh katika Swahiyh Al-Jaami' 7565)]

 

Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Raka'ah mbili baada ya Witr [At-Tirmidhiy na wengineo, As-Sunan 433]

 

An-Nawawy kasema kwamba rai iliyokuwa sahihi ni kwamba alikuwa akiswali Raka'ah mbili baada ya Witr kwa kukaa kuonyesha kwamba hivi inaruhusiwa na hakufanya hivyo kila mara  [Tuhfat Al-Ahwadhi Sharh Jaami' At-Tirmidhiy].

 

Sunnah ni kwamba Swalaah ya usiku ya Muislamu imalizikie na Witr kutokana na Hadiyth ya Al-Bukhariy 943, lakini kama ameswali na Imaam na amependa kuswali zaidi nyumbani khaswa siku za baridi, basi aswali kama tulivyobainisha mwanzo.

Kuhusu idadi ngapi ya Raka'ah kuswaliwa usiku, Sunnah ni kuswali Raka'ah kumi na moja kutokana na Hadiyth iliotoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa)  ((….Hajapata kuswali zaidi ya Raka'ah kumi na moja katika Ramadhwaan wala katika miezi mingine))  [Al-Bukhaariy 1874]

 

Na njia bora kabisa ya kuswali Swalaah ya usiku ni kuziswali Raka'ah mbili mbili na kuziswali Raka'ah mbili za Witr pekee yaani kutokuinga na moja ya mwisho (bali moja ya mwisho iswaliwe pekee yake na sio kuziunga zote tatu pamoja)  kutokana na Hadiyth iliotoka kwa  Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali usiku Raka'ah mbili mbili kisha akimalizia kwa Raka'ah moja)) [Al-Bukhaariy, al-Fath, 940].

 

Hii ndio njia bora kabisa ya kuswali Swalaah ya usiku inayojulikana kutokana na Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na pia zipo njia nyingine tofauti za kuswali ambazo zinazojulikana vilevile.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share