Mchuzi Wa Kuku Na Viazi Bila Ya Nyanya (Trinidad/Guyana)

 

Mchuzi Wa Kuku Na Viazi Bila Ya Nyanya (Trinidad/Guyana)

 

 

Vipimo

 

Kuku 1

Vitunguu – 5 saizi ya kiasi

Viazi – 4  

Tangawizi mbichi ilokunwa 1 kijiko cha kulia

Kitunguu thomu (saumu) kilosagwa – kijiko 1 cha kulia

Pilipili boga (capsicum) la kijani – ½

Majani ya nanaa (mint) – mche 1

Kotimiri – kiasi

Kitunguu cha kijani kichanga (spring onion) – mche 1

Pilipili mbichi  ukipenda - 2

Bizari ya mchuzi – vijiko 2 vya kulia

Chumvi - kiasi

Ndimu – ½

Mafuta ya kupikia kiasi ya robo kikombe.

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Msafishe kuku, umkatekate vipande vya kiasi. Kisha mweke katika bakuli uchanganye na tangawizi mbichi, thomu, chumvi. Mroweke kwa muda kiasi.
  2. Menya viazi ukatekate vipande.
  3. Menye vitunguu ukatekate slaisi ndogo ndogo au vipande vidogodogo.
  4. Weka, pilipili boga, nanaa, kotimiri, kitunguu cha kijani, pilipili mbichi katika mashine ya kusagia (blender) usage kwa maji kidogo sana.
  5. Weka bizari ya mchuzi katika kibakuli kidogo, changanya na maji kiasi ya robo kikombe.  
  6. Weka mafuta katika sufuria yakishika moto, mimina bizari ya mchuzi uliyochanganya na maji ukaange kwa dakika moja kiasi.
  7. Tia vitunguu, kakaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (golden brown).
  8. Tia kuku uchanganye vizuri na uendelee kukaanga humo katika sufuria.
  9. Tia viazi endelea kidogo kukaanga, kisha tia maji kiasi ufunike kuupika mchuzi na kuku na viazi viwive.
  10. Koleza chumvi na ndimu ikiwa tayari.

 

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Kidokezo:

 

Kulia na wali au:

 

Roti- Chapatti Za Trinidad Na Guyana

 

 

 

 

 

 

Share