Imaam Ibn Baaz: Wakati Maalumu Wa I’tikaaf Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je Inajuzu Kuikata?

Wakati Maalumu Wa I’tikaaf Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajuzu Kuikata?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

15. Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajuzu Kuikata?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. Kauli ya sahihi kabisa ya Ahlul-‘Ilm ni kwamba haina wakati maalumu.

 

b. Na Sunnah ni mtu aingie akiwa Mu’takif  pindi anapotia niyyah kwa ajili ya I’tikaaf na atoke baada ya kumaliza muda wake alionuia.

 

c. Na anaweza kuikata ikiwa atahitaji kufanya hivyo kwa sababu I’tikaaf ni Sunnah haipasi kujiwajibisha nayo ikiwa ni mwenye udhuru.

 

d. Na I’tikaaf inapendekezeka katika makumi ya mwisho ya Ramadhwaan na ni mustahabu kwa mwenye kuingia I’tikaaf aingie akiwe Mu’takif baada ya Swalaah  ya Alfajiri kuanzia siku ya ishirini na moja, kama alivyofanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atoke inapomalizika masiku kumi (ya mwisho). 

 

 

[Majmu’w Al-Fataawaa (15/442)]

 

 

Share