Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Swalaah Ya ‘Iyd Inavyoswaliwa

  Swalaah Ya ‘Iyd Inavyoswaliwa

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

i-Inaletwa Takbiyrah Al-Ihraam na inafunguliwa kwa du’aa kisha zinaletwa Takbiyrah sita (jumla zitakuwa saba) kisha inasomwa Al-Faatihah na Suwrah ima (Sabbihisma) au (Qaaf) katika Raka’ah ya kwanza. 

 

ii-Katika Raka’ah ya pili, atakaposimama kutoka katika kusujudu, atainuka huku akileta Takbiyrah kisha ataleta Takbiyrah tano baada ya kusimama kwake. Kisha atasoma Al-Faatihah na Suwrah. Ikiwa atasoma katika Rakaa ya kwanza (Sabbihismaa) basi asome katika Rakaa ya pili (Al-Ghaashiyah). Na pindi akiwa amesoma katika Rakaa ya kwanza (Qaaf), basi asome katika Rakaa ya pili (Iqtarabatis-Saa’ah .. Suwrah Al-Qamar)

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/223)]

 

Share