Imaam Ibn Al-Qayyim: Mwenye Kuacha Swalaah Ya Ijumaa Allaah Ataupiga Mhuri Moyo Wake

Mwenye Kuacha Swalaah Ya Ijumaa Allaah Ataupiga Mhuri Moyo Wake

 

Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Swalaah ya Ijumaa ni katika fardhi za Uislamu zilizosisitizwa, na ni miongoni mwa mikusanyiko mitukufu ya Waislamu. Nao ni (mkusanyiko) mtukufu kuliko mkusanyiko wowote wanaokusanyika (Waislamu) ndani yake.  Na ni wa faradhi zaidi kuliko (mikusanyiko) yote isipokuwa (mkusanyiko) wa 'Arafah.

 

Atakayeiacha kwa kupuuza (bila ya udhuru unaokubalika ki-Shariy’ah), basi Allaah Ataupiga mhuri moyo wake.”

 

 

[Zaad Al-Ma’aad (1/376)]

 

 

Share