020-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Je, Kuna Wakati Maalum Wa Kukata Kucha, Kukata Sharubu, Kunyofoa Nywele Za Kikwapa Na Kunyofoa Kinena?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Twahara

 

020-Je, Kuna Wakati Maalum Wa Kukata Kucha, Kukata Sharubu,

Kunyofoa Nywele Za Kikwapa Na Kunyofoa Kinena?

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Mambo haya hayana wakati  maalumu wa kuyafanya, bali kinachoyadhibiti ni haja. Wakati wowote mtu anapohisi kwamba anahitajia kulifanya moja wapo, basi huo ndio wakati wake. La muhimu ni kuwa mtu asijiachie zikapita zaidi ya siku arobaini bila ya kufanya chochote. Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Anas aliyesema:

 

((Tumewekewa muda wa kuwa tusiachie zikapita siku zaidi ya arobaini bila kukata sharubu, kukata kucha, kunyofoa nywele za kikwapa na kunyoa kinena)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (275) na wengineo].

 

 

 

Share