Skip to main content

01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ اَلطَّهَارَةِ - Kitabu Cha Twahara035-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Kupaka Juu Ya Vizuizi

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

Mlango Wa Twahara

035-Kupaka Juu Ya Vizuizi 

Kwanza: Kupaka Juu Ya Khufu Mbili

Alhidaaya.com

Taarifu yake: Khufu ni viatu vya ngozi vinavyofunika visigino viwili. [Nayl Al-Awtwaar (1/241)].

Na kupaka kilugha ni kisoukomo (masdwar) cha kitenzi cha “amepaka”, nako ni kuupitisha mkono juu ya kitu kwa kuukunjua. [Al-Qaamuws Al-Muhiyt na Maqaayiys Al-Lughah].

 Na kupaka juu ya khufu mbili maana yake ni kuitia umajimaji khufu maalumu katika wakati na mahala maalumu badala ya kuosha miguu miwili wakati wa kutawadha. [Ad-Durru Al-Mukhtaar].