043-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Mahala Pa Kupukusa Na Sifa Yake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Twahara

 

043-Mahala Pa Kupukusa Na Sifa Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

Linalo ruhusika kisharia, ni kuzipukusa khufu mara moja tu nje (juu)  na sio ndani (chini ya unyayo). Hii ni kwa Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib aliyesema: “ Lau kama dini ingelikuwa ni kwa rai, basi kupukusa chini ya khufu ingelikuwa ni bora kuliko juu yake. Na hakika nilimwona Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akipukusa juu ya khufu zake mbili”.[Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (162), Ad-Daara Qutwniy (73) na Al-Bayhaqiy (2/111). Tazama Al-Irwaa (103)].

 

Na haya ni madhehebu ya Ath-Thawriy, Al-Awzaa’iy, Ahmad, Abuu Haniyfay na wenzake. Na haya ndio sahihi.  [Ikhtilaaf Al-‘Ulamaa (uk.30), Masaail Ahmad cha Ibn Haaniy (1/21), Al-Awsatw (1/453) na Al-Muhalla (2/111)].

 

Maalik na Ash-Shaafi’iy wamesema: “Hupukusa juu yake na chini yake. Na kama atapukusa juu tu, basi itamtosheleza. [Nihaayat Al-Muhtaaj (1/191), Al-Mudawwanah (1/39) na Al-Khurshiy (1/177)].

 

Hili limetolewa dalili kwa Hadiyth ya Al-Mughyrah bin Shu’ubah aliyesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha, kisha akapukusa chini na juu ya khufu zake. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (165), At Tirmidhy (97), Ibn Maajah (550) na Ahmad (4/251). Ahmad, Al-Bukhaary, Abuu Haatim, Ad-Daara Qutwniy na Ibn Hajar wamesema ina dosari].

 

Hii ni kauli dhwa’iyf, lakini lililo na uthibitisho toka kwa Al-Mughyrah ni kauli yake isemayo: “Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akipukusa juu ya khufu zake mbili”.[Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (161), At Tirmidhy (98) na wengineo].

 

Hivyo basi, haifai kupukusa isipokuwa juu ya khufu mbili tu. Na kama atapukusa chini tu akaacha juu, basi kupukusa huko hakutatosheleza. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

Share